‘Cardiac Arrhythmia’ ni pale mtu anapokuwa na mapigo ya moyo yasiyo ya
kawaida au yanayodunda sana. Mwili una mfumo asili wa umeme unaosaidia
moyo kufanya kazi. Mfumo huu husababisha moyo kutanuka na kusinyaa
ambapo husababisha damu kuingia na kutoka kwenye moyo; umeme kwa kawaida
hufuata mkondo na mapigo ya moyo kwa kasi ya kawaida. Ingawa, kama
mkondo wa kawaida wa umeme huu ukivurugwa moyo hushindwa kufanya kazi na
kusababisha mapigo ya moyo ama kwenda taratibu sana, haraka sana au
yasiyoimara.
Kuna
aina kadhaa za ‘Arrhythmia’; Baadhi ni pamoja na zijulikanazo kitaalamu
kama Supra-Ventricular Tachycardia, Ventricular Tachycardia,
Ventricular Fibrillation, Atrial flutter and Atrial Fibrillation.
Mapigo
ya moyo yasiyo imara hasa husababishwa na ugonjwa wa moyo na moyo
kushindwa kufanya kazi. ‘Arrhythmia’ ndogo pia huweza kusababishwa na
mtindo wa maisha usiozingatia afya bora ikiwa ni pamoja na uvutaji
sigara uliopitiliza, Ulevi na kuzidisha matumizi ya kafeini au msongo wa
mawazo.
Ingawa
imegundulika hasa katika uchunguzi wa mara kwa mara wa matibabu dalili
za ‘arrhythmia’ ni chache zinazoweza kuonekana ikiwa ni pamoja na
kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kupungua kwa mapigo ya moyo, maumivu ya
kifua, kizunguzungu, kuchoka sana na kukosa pumzi.
‘Arrhythmia’
mara nyingi hutokea kwa nyakati tofauti tofauti. Hali ya kutotabiri kwa
‘arrhythmia’ na kutokea kwake kwa nyakati tofauti tofauti hufanya
uchunguzi kuwa mgumu. Moja ya vifaa vitumikavyo zaidi kwa uchunguzi wake
kitaalamu ni ‘electrophysiology (EP)’ na kinachukuliwa kuwa bora zaidi
katika taaluma hii.
Utafiti
wa EP hufanya kazi kwa kupima na kurekodi shughuli za umeme wa moyo na
kuonesha njia za umeme. Inaonesha sababu na mahala penye tatizo la
mapigo ya moyo. Matatizo yanayotokea katika utafiti wa EP ni machache
sana kwa kuwa umekuwa ukifanyika salama kwa miaka mingi sasa.
Taarifa
inaweza kuundwa katika namna mbili, ama kupitia ramani ya shughuli za
umeme wa moyo kupitia kifaa maalumu kitaalamu ‘electrocardiogram (ECG)’
inayoonesha wapi ishara zisiyo za kawaida zinaanza kutokea ndani ya
moyo.
Mfumo
wa wa kitaalamu wa ‘Carto3’ ujulikanao kama ‘3D mapping’ ni teknolojia
mpya inayotoa muonekano wa moyo kwa ukubwa mara tatu zaidi. Hii
hupelekea kuboreshwa kwa usahihi wa vipimo na matibabu ya mgonjwa.
Kwa
kesi ya kushuka kwa mapigo ya moyo, utafiti wa EP unatoa nafasi
kutathmini haja ya vifaa kama vile ‘peacemaker’ au ‘defibrillator’
ambavyo husaidia kuzuia vifo vya ghafla vya magonjwa ya moyo.
Baada
ya uchunguzi kupitia utafiti wa EP, mirija maalum ya ‘Radiofrequency
(RF) catheter ablation’ huingizwa katika mishipa ya damu ambapo viwango
vya juu na vya chini vya mzunguko wa nguvu ya umeme vinapokelewa katika
tishu za moyo na kuharibu tishu zile zinazohusika na mapigo ya moyo
‘arrhythmia’. Baada ya matibabu kwa kawaida wagonjwa sasa huweza
kikamilifu kupunguza matumizi ya dawa ambapo mgonjwa ataweza kupumua
vizuri na mapigo ya moyo kwenda vizuri.
kwa
mujibu wa Dkt A M Karthigesan wa hospitali za Apollo baadhi ya
‘arrthythmia’ zilitibiwa kupitia kipimo maalumu kijulikanacho kitaalamu
kama ‘RF Ablation’ ni ‘Supraventrical Tachycardia (SVT’; hii inatokea
kwenye vyumba vya juu vya moyo na kwa ujumla inaelezewa kama moyo kupiga
kwa kasi. Pingili za ‘Atirioventrikali (AVNRT)’, ‘atirioventrikali
reentry (AVRT)’ na ‘focal atrial tachycardia’ ni baadhi ya aina nyingi
za SVT.
Zaidi
‘Atrial Flutter (AFL)’ inaweza pia kutibiwa kwa upasuaji wa RF. AFL ni
wakati atria inapopiga haraka sana kwa kiwango cha karibu mapigo 300 kwa
dakika yanayotokea katika chumba cha juu cha moyo.
Arrhythmia
nyingine maarufu inayotibiwa kwa RF ni ‘Atrial Fibrillation (AF)’. Hii
ni wakati uwezo wa moyo kufanya kazi zake unapunguzwa kwa mapigo yasiyo
na mpangilio ya chumba cha juu cha moyo. Ingawa ‘atrial fibrillation’
haitishii maisha, kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kupelekea
matatizo kama vile damu kuganda ambapo hatimaye inaweza kusababisha
kiharusi.
Mwisho
‘Ventricular Tachycardia (VT)’ ambayo kama ikiachwa bila kutibiwa
inaweza kuwa aina ya ‘Arrhythmia’ ya kuhatarisha maisha, hii hutokea
wakati chumba cha chini cha moyo kikimpiga kwa kasi sana
Dkt.
A M Karthigesan wa hospitali za Apollo anasema kuwa baadhi ya manufaa
ya kufanyiwa tiba ya upasuaji kwa mirija ni kuwa mtu atarajie mabadiliko
ya haraka katika ubora wa maisha sababu ya kuongezeka kwa uwezo wake wa
kufanya kazi; Huduma ya matibabu iliyoboreshwa kwa jinsi mgonjwa
anavyohitaji imeondoa upotevu wa muda; Kupungua kwa gharama za tiba na
kuokoa maisha ambapo mgonjwa anapewa nafasi nyingine ya kuishi.
Imechangiwa na:
Dkt A M Karthigesan
Mshauri wa tiba ya umeme wa moyo
Hospitali za Apollo, Chennai
No comments:
Post a Comment