Na Mwandishi Wetu,
Novemba
14 kila mwaka tunaadhimisha siku ya kisukari duniani ili kuongeza
uelewa kuhusu madhara ya kisukari, matatizo yanayoletwa na huu ugonjwa
na taarifa muhimu kuhusu kisukari.
Siku
hii inabeba ujumbe mahususi kwa watu wote ulimwenguni. Kauli mbiu
katika siku hii tokea 2014 hadi 2016 ni maisha bora na kisukari(healthy
living and diabetes) na mwaka huu kuna mtazamo zaidi katika kuzingatia
mlo kamili na kuanza kila siku na kifungua kinywa bora
.
.
Kutoka
katika shirika la kisukari Africa, Tanzania ni kati ya nchi 32 katika
shirikisho hilo kwa viwango vya nchi zenye viwango vya kisukari duniani.
Kulikuwepo na zaidi ya kesi milioni 1.7 za kisukari hapa Tanzania kwa
mwaka 2014. Shirika la afya duniani (WHO) linakadiria zaidi ya watu
milioni 180 ulimwenguni wana kisukari, na hiyo takwimu inatarajiwa
kuongezeka ifikapo mwaka 2030 kama hamna hatua yoyote itakayochukuliwa.
Kifungua
kinywa bora na sahihi kitasaidia sana kiwango cha sukari mwilini
kutokuwa juu sana wala chini sana na kukuweka vizuri kutokea asubuhi.
Katika maadhimisho ya siku ya kisukari dunia, kliniki ya sukari kutoka hospitai za Apollo imeandaa siku 2 za kupima na kuhamasisha katika kambi iliyopo hospitali za Apollo
kuwaasa watu kuhusu mifumo na staili za maisha yao ili kujikinga na
kisukari. Kambi hiyo itakuwa na; vipimo vya sukari katika damu,
mchanganuo wa mafuta mwilini, na namna ya kuepuka kisukari ambapo hospitali za Apollo
zitatoa somo kuhusu milo kamili kutoka kwenye timu yao ya wataalam wa
milo. Wataalam hao watafundisha namna ya kujikinga na kisukari kwa
kuzingatia milo bora, namna ya kudhibiti kiwango cha sukari mwilini na
namna ya kupambana na kisukari kwa ujumla.
Kwa kuona umuhimu wa kutoa huduma hiyo ya kisukari kupitia elimu ya mlo, Dk. Bhuvaneshwari Shankar Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo, ana
lengo la kuwaelimisha watanzania kuhusu mambo muhimu wanapaswa kuyajua
kuhusu kisukari na mlo kamili katika siku hii ya kisukari duniani.
Kula
kwa afya ni silaha bora kujikinga na kisukari. Mazoezi ya mara kwa mara
na mlo kamili vinasaidia sana. Hamna chakula mahususi au mfumo mgumu wa
lishe unaohitajika.
Dk Bhuvaneshwari Shankar anatutia moyo kula milo mitatu kama inavyostahili kitu ambacho watanzania wengi hatufanyi hivyo.
“muda
mrefu bila chakula kunafanya sukari kushuka, na utajikuta unakula
chakula kingi ambacho kitapelekea sukari katika damu kutokuwa sawa. Alisisitiza
Ratiba
nzuri ya chakula cha mtu wa kisukari kinatakiwa kiwe na mafuta kidogo,
mboga mboga, katika siku ni muhimu. chakula kingi kinanafanya sukari ya
mwili kutokuwa sawa. Angalizo linahitajika katika uchaguzi sahihi wa
vyakula.
Katika chaguo sahihi la vyakula “Dk Shankar wa hospitali ya Apollo anasisitiza umuhimu wa watanzania kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwa kufuata mlo sahihi.
”chagua
vyakula vyenye nyuzinyuzi, na kabohaidreti ndogo ni muhimu. Epuka
bidhaa nyingi zilizochujwa nyuzi zake, ila chagua unga. Unga ulio na
virutubisho vyote ni wa muhimu. Dhibiti kiwango cha mafuta kuingia
mwilini, na epuka mafuta yaliyotengenezwa.
Ule milo 3 kwa siku na vitafunwa hapo katikakati. Chagua milo yenye
nyuzinyuzi sana zaidi ya ile yenye kabohaidrates, mbogamboga zenye
stachi Epuka chokleti, barafu tamu zenye mafuta na sukari nyingi. Chagua
samaki wazuri na kuku wakuchemsha sio kukaangwa na mafuta. Chagua
maziwa yenye mafuta kidogo.
Dumisha uzito unaopaswa kwa kufanya mazoezi kwa kutembea na kula katika muda muafaka, alisisitiza Dk. Shankar.
Kisukari
ni ugonjwa unaoathiri watu katika umri wowote ambapo mwili unashindwa
kutengenzea sukari ya kutosha au kushindwa kutumia inslulini
iliyotengezwa hivyo kupelekea kiwango cha sukari mwlini kutodhibitiwa.
Mwili wa mwanadamu unapata sukari kutoka kwenye sehemu kuu mbili; kwanza
kutoka kwenye vyakula tunavyokula, pili kutoka kwenye ini
linalotengeneza pindi unapokuwa hujala chakula. Mwili unabadilisha hii
sukari na wanga kwenda na kuwa nguvu kwa kutoa homoni zinazoitwa insulin
zinazotengenezwa na kongosho.
Kuhusu Hospitali za Apollo
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira
yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea
kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya
jamii ya kibinadamu".Katika miaka 30 tokea
kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata
kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la
Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini
india.
Katika
safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka
nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya
upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000
za mishipa myembamba.Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha
idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na
zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india,
zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji
unaotumia mashine za kiroboti.
No comments:
Post a Comment