Na Mwandishi wetu,Dar es salaam
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini
umekanusha kuwepo kwa madai yaliyotolewa na Hospital ya Rufaa Mkoani Mbeya kuwa wanaudai Mfuko jumla ya shilingi bilioni 2 na
kwamba wanaudai Mfuko kutoka mwezi Juni,
2015.
2015.
Akizungumza jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya Ndugu Michael Mhando amesema madai
yaliyotolewa na Hospital hiyo ya Rufaa Mkoa wa Mbeya hayana ukweli wowote nakwamba mfuko huo unalipa madai baada ya mtoa huduma kuwasilisha
kwenye Mfuko.
Amesema madai ya mwisho ya Hospitali hiyo kulipwa ni ya
mwezi Agosti, 2015. Madai ya mwezi Septemba, 2015 yamewasilishwa kwenye Mfuko
tarehe 4/11/2015 ambayo mpaka sasa yana siku 15 tu. Kwa hiyo Hospitali ya Rufaa
ya Mbeya tumewalipa madai yao yote na kwa mwaka huu wa 2015 kuanzia Januari
hadi Agosti 2015 tumewalipa kiasi cha shilingi bilioni 4.3.
Madai mengi ambayo yamekuwa yakiwasilishwa kwao yamegubikwa na udanganyifu
mkubwa hali inayowafanya kuchukua muda mrefu katika uhakiki wake ikiwemo
kuwapigia simu wagonjwa waliopewa huduma za matibabu.
Aidha Mhando amesema mfuko huo unatoa onyo kali kwa watoa huduma ambao
wamekuwa bado wakijihusisha na udanganyifu wa aina yoyote kwa kuwa haitawaonea
haya kuwafutia usajili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Amesema Mfuko pia unazidi kutoa rai kwa watoa huduma kutumia fursa
zinazotolewa na Mfuko katika kuhakikisha huduma za matibabu zinaboreshwa kwa
wanachama na Watanzania kwa ujumla.
Wakati huo Kaimu mkurugenzi huyo
amesema Katika kipindi hiki, baadhi ya watoa huduma wamekuwa wakitoa sababu
mbalimbali za kushindwa kutoa huduma nzuri ama za kuridhisha kwa wanachama
wao na wananchi kwa ujumla kwa
kisingizio cha kukosa fedha hali inayosababisha kukosa dawa, kukosa vifaa tiba
na vitendanishi pamoja na kushindwa kuboresha mazingira ya vituo.
Watoa huduma hao wanadai hayo ama wanatoa visingizio vya kukwama huduma
katika maeneo yao kutokana na NHIF kuchelewa kulipa fedha fedha za madai ambayo
wametibia wanachama wake.
Amesema taarifa hizo zinajenga
mazingira kuwa NHIF ni kikwazo katika ufanisi wa vituo hivyo jambo ambalo si la
kweli na limebeba taswira ya kuleta chuki baina ya wanachama ama wananchi na
chombo chao ambacho kina dhamana ya kuwatibia.
Hata hivyo Mhando amekanusha kuwa wao
ndio kikwazo ama sababisho la huduma mbovu katika vituo hivyo nah ii
inatokana na ukweli kwamba zipo jitihada mbalimbali ambazo NHIF imekuwa
ikizifanya kuhakikisha inasaidiana na Serikali katika kuboresha huduma za vituo
hivyo ili wananchi kwa pamoja wapate huduma zinazostahili.
MWISHO.
(Imeandaliwa na Mtandao wa www.Jamiimoja.blogspot.com-0759406070)
No comments:
Post a Comment