Monday, November 23, 2015

WADAU WAJITOKEZA KUISAIDIA TIMU YA KIKAPU MBEYA



 Na EmanuelMadafa,Mbeya
Wachezaji 22 wa mpira wa kikapu Mkoa wa Mbeya, tayari wamefanikiwa kuondoka mkoani humo kwa ajili ya  kushiriki mashindano ya Taifa CUP, yatakayofanyika  Mkoani Dodoma  November 22 hadi November 30 mwaka huu.



Wachezaji hao walishindwa kusafiri mapema kuelekea mkoani Dodoma

 kushiriki mashindano hayo  kutokana na kukabiliwa na uhaba wa fedha hali iliyofanya kuwepo na maandalizi hafifu.



Aidha kufanikiwa kwa timu hiyo kunatokana na
kujitokeza kwa  Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola, Mkoa wa Mbeya pamoja na Kampuni ya Tbl , amboa wamechangia kiasi kidogo cha fedha kilicho fanikisha safari hiyo.



Akizungumzia juu ya kupokea kwa ufadhiri huo Katibu wa chama  cha mpira wa kikapu mkoani Mbeya ambaye pia ni mwalimu wa timu hiyo  , Yusuf Nyirenda, amesema kuwa wanawashukuru wadau hao kwa kujitokeza   kwa kuchangia kiasi hicho cha fedha .



Amesema kampuni ya  Coca Cola pekee imechangia kiasi cha shilingi Mil 1.5 ambapo kwa upande wa Tbl  wamechangia kiasi cha shilini laki tano   hivyo watajitahidi kutumia kaisi hicho kilicho patikana  ili kushiriki mashindano hayo.



Amesema, tayari timu imekwisha ondoka   Mbeya November 21, ikiwa na wachezaji 22 kati yao wanawake 11 na wanaume 11 lakini mpaka sasa  wamefanikiwa kupata shilingi milioni 2  kati ya milioni 4,700,000 zinazohitajika.



“Kiasi cha shiringi milioni 4,700,000 zinahitajika kwa ajiri ya usafiri wa kwenda na kurudi, chakula, malazi na ada ya kushiriki mashindano haya,”alisema.



Amesema kwa dhati kabisa anaipongeza kampuni ya Coca cola kwani ndio kampuni pekee ambayo imekuwa ikijitoa mara kwa mara kusaidia timu hiyo .



Amesema kutokana na mazingira hayo baadhi ya wachezaji watalazimika kujigharamia wenyewe katika eneo la usafiri   hivyo, amewaomba wadau  na mashabiki wa mpira huo, kuendelea kjitokeza kwa wingi katika kuichangia timu hiyo ili iweze kushiriki mashindano hayo.



Mwisho.
( Imeandaliwa na Mtandao wa www.Jamiimoja.blogspot.com- Mbeya 0759406070)

No comments: