Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky
Sadiki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro
iliyokuwa na kaulimbiu “ Weka Mlima Safi, Tunza Mazingira Yakutunze”
katika lango la Marangu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kati) na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya
Kilimanjaro Betrita Loibooki.
Wakurugenzi kutoka TANAPA wakifuatilia uzinduzi
wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa
Uhifadhi Mtango Mtahiko, Mkurugenzi Utumishi na Utawala Bi. Witness Shoo,
Mkurugenzi wa Mipango Dk. Ezekiel Dembe,
Mkurugenzi wa Fedha Nassoro
Mndeme na nyuma yake Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Ibrahim Mussa.
Wanafunzi kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori
Pasiansi Mwanza nao walishiriki katika kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita
Loibooki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usafi Mlima
Kilimanjaro.
Baadhi
ya wadau walioshiriki kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky
Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA pamoja na wadau
kutoka Kampuni mbalimbali za mawakala wa utalii kutoka Kilimanjaro na
Arusha wanaoshiriki Kampeni maalum ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky
Sadiki akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima
Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete
akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima
Kilimanjaro.
Mazingira
safi yataendelea kuufanya Mlima Kilimanjaro kutiririsha maji kwa wingi zaidi.
Na Dixon Busagaga waGlobu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment