Friday, April 29, 2016

Tigo yatoa visima 12 vya maji kwa vijiji 12 Singida

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akikata utepe katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akifungua moja ya bomba katika kisima   katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
 Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) akifungua bomba katika moja ya kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo pembeni yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mtinko  katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 

Singida, Aprili 27th 2016:  Kampuni ya simu ya Tigo leo imekabidhi visima 12 vya maji  vyenye thamani ya 174m/- kwa vijiji 12 mkoani  Singida  ikiwa ni kuchangia juhudi za serikali  za kupunguza  uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano  iliyofanyika kwenye kijiji cha Mtinko wilayani Singida  mkoani Singida, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata  alisema ufadhili huo  umo kwenye mikakati ya kampuni ya kusaidia  jamii katika kunyanyua hali zao za maisha.
 Vijiji vitakavyonufaika kutokana na ufadhili huo pamoja na wilaya zake kwenye mabano ni Lulumba (Iramba), Kisana (Iramba), Kisonzo (Iramba), Songambele (Iramba), Kinyeto (Singida Vijijini) na  Damankia (Ikungi). Vingine ni  Muungano (Ikungi), Ighuka (Ikungi), Kamenyanga (Manyoni), Sasajila (Manyoni), Mtinko (Singida Vijijini) and Kinampanda (Kinampanda).
 “Msaada huu ni sehemu ya uwekezaji wa Tigo kwenye miradi ya kijamii  ambayo inaleta tija kubwa kwa jamii. Tuna imani kwamba kupitia visima hivi, Tigo inasaidia  kutatua uhaba mkubwa wa maji  katika eneo hili la mkoa wa Singida  ambalo kwa kiwango kikubwa  limekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua katika kipindi cha miaka mine  iliyopita,” alisema Lugata.
 Aidha aliongeza kuwa uhaba wa maji  miongoni mwa  wilaya nyingi za Singida  umesababisha wakiazi wake  kupoteza muda mwinmgi kutafuta  bidhaa hiyo muhimu, jambo ambalo  Tigo inaamini  kuwa hivi sasa litafikia ukomo kutokana na upatikanaji wa visima hivyo.
 Makabidhiano ya visima hivyo yalihudhuriwa na kushuhudiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge  ambaye aliishukuru Tigo kwa ufadhili huo uliopatikana kwa wakati mwafaka akisema kwamba visima hivyo vitapunguza kwa kiwango kikubwa  uhaba sugu wa maji  uliolikumba eneo hilo  na kuchangia kukua ustawi wa jamii  kijamii na kiuchumi.
 Hata hivyo, alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo  kuchangia kwenye juhudi kama hizo. Waziri Lwenge alisema, “Tunatoa shukrani za dhati kwa Tigo kwa kutuunga mkono kwenye juhudi zetu za kutatua  uhaba wa maji uliopo Singida na hata kwenye mikoa mingine nchini. Tuna imani visima hivi 12  vitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili linaloikabili jamii kwa sasa”.



No comments: