Monday, September 12, 2016

BEI YA SAMAKI SOKO LA FERI JIJINI DAR ES SALAAM YASHUKA

 Wachuuzi wa Samaki wakisubiri kununua kitoweo hicho katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Bei ya samaki katika soko hilo imepungua kutokana kwa kupatikana kwa wingi kwa kitoweo hicho.
Mnada wa samaki ukiendelea

Na Dotto Mwaibalae

HALI ya bei ya samaki katika Soko la Kimataifa la Feri jijini Dar
es alaam imeshuka kutokana na samaki kupatikana kwa wingi katika kipindi cha mwezi wa Septemba.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com jijini Dar es Salaam leo asubuhi mchuuzi wa samaki katika soko hilo Mohamed Hassan alisema katika kipindi cha wiki mbili bei ya samaki imeshuka ukilinganisha ni mwezi uliopita.

"Sasa hivi samaki aina ya King Fish, Changua wanauzwa kati ya sh.30,000 lakini kipindi ambacho wakiadimika ufikia hadi sh.35,000" alisema Hassan.

Mchuuzi mwingine wa samaki katika soko hilo Shabani Shamte alisema samaki aina ya kibua, ngisi wakati huu uuzwa kati ya sh. 23,000 hadi 25,000 ambapo wakiadimika ufikia hadi sh. 30,000.

Grace Tesha ambaye uuza samaki hao maeneo ya Mabibo Loyola alisema hata wao kipindi hiki biashara yao inakwenda vizuri kutokana na kuwepo kwa samaki wengi.

"Samaki wakiadimika huwa inatuwia vigumu mno kibiashara kwani wateja wetu wamekuwa wakilalamia kuwauzia kwa bei kubwa" alisema Tesha

No comments: