Sunday, September 11, 2016

DC STAKI: APIGA MARUFUKU KUFANYA BIASHARA KWA KUJAZA RUMBESA

Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akikagua magunia yaliyokutwa yakiwa yamejazwa Rumbesa
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akizungumzia unyonyaji wanaokumbana nao wananchi kutoka kwa wafanyabiashara wanaotaka magunia yaliyojazwa Rumbesa

Gari aina ya Fuso likiwa limekamatwa mara baada ya kubainika kuwa limebeba magunia ya vitunguu ambayo yamejazwa Rumbesa

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anna-Claire Shija akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wananchi Wilayani humo

 Dc Staki akikagua mashamba ya wakulima mara baada ya kuzuru katika maeneo hayo


 Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo wakisikiliza malalamiko ya wananchi

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Wakulima wa mazao mbalimbali likiwemo zao la vitunguu wametakiwa kutofanya biashara kwa kujaza rumbesa ili kuwanufaisha wafanya biashara ambao wanajitokeza vijijini kunua mazao kwani jambo hilo linawanyonya zaidi wakulima na kuwanufaisha wafanya biashara.

Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule mara baada ya kuitisha mkutano wa wananchi katika ziara yake ya kuwahimiza kwa pamoja kujitokeza kushiriki katika zoezi la upimaji ardhi linaloendeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Same.

Hata hivyo lengo mahususi la kuamua kuwapo kwa zoezi la upimaji ardhi ni kutaka kuondoa migogoro ya ardhi iliyokithiri katika maeneo mbalimbali Wilayani humo sambamba na kupinga kipimo cha Rumbesa kinachowanyonya wakulima wengi nchini.

Katika mkutano huo uliofanyika Katika Kitongoji cha Jitengeni na Mvungwe uliwahusisha pia wataalamu wa kilimo na ardhi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo sambamba na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo.

Katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wakazi wa Kijiji cha Ruvu Jiungeni kushiriki kikamilifu katika zoezi la upimaji ardhi hivyo kuwaarifu pia wananchi wote kujitokeza katika mashamba yao wakati wa zoezi la upimaji ili kuondoa adha inayochochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Dc Staki alisema kuwa wananchi wanapaswa kupinga kuzidisha kipimo halisi kinachokubalika kwani kutofanya hivyo ni kukubali kupunjwa na kuinyima Halmashauri mapato.

Alisema kuwa wakulima wanapaswa kujiamini kwani mazao wanayolima yana soko popote nchini hivyo kidanganywa kwa kuweka Lumbesa ni kujinyima haki yao ya msingi katika kukabiliana na wimbi la umasikini.

Aidha kabla ya mkutano na wananchi Dc Staki alitembelea mashamba ya vitunguu na kujionea jinsi ambavyo Rumbesa inavyofungwa.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya alimtaka mkuu wa Polisi Wilaya ya Same Asteriko Maiga kusimamia na kulikemea suala la Rumbesa kwenye mageti yote na endapo watawabaini wafanya biashara wanaofanya hivyo wanapaswa kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anna-Claire Shija alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini katika kuimarisha kilimo na kujitokeza kwa wingi katika shughuli za maendeleo.

No comments: