Sunday, October 23, 2016

KAMPENI YA KUPIGA VITA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI YA BINTI WA KITAA YAFANYIKA TABATA JIJINI DAR

Bibi Pili Abdallah akielezea kwa kina maisha ya Mabinti wadogo yanayowapelekea kupata Mimba za utotoni na kuolewa wakiwa wadogo, pia alizungumzia Tamaa na Matamanio yalivyo na nguvu ya kuwafanya watoto wakike kujiingiza katika maswala ya ngono wakiwa wadogo na kupelekea kupata mimba, mwisho aliwashauri wazazi wenzake kuwatambua watoto  wao.
Furahini Michael akiulizwa swali na Bwana Steven Mfuko kuhusu athari za mimba za utotoni na kuolewa katika
umri mdogo.
 Mkazi wa Tabata kwa Cecy ambapo kampeni ya Binti wa kitaa ilifanyika Bi.Sheira Mheni akielezea jinsi watoto hususani wa kike wenye umri kati ya Miaka 12-17 walivyoharibika kutokana na mabadikiko ya Teknolijia ambapo imewapekea kufahamu mambo ya wakubwa wakiwa watoto na hatimaye kupata matamanio na kufanya kama walivyo ona katika Mitandao ya kijamii na Runinga jambo linalowasababishia Mimba za Utotoni
 Mwenyekiti  wa Serikali ya Mtaa wa Tenge Athuman Mpwenewe akieleza namna ambavyo kumekuwa na Mimba nyingi za utotoni katika mtaa wake na juhudi ambazo zimefanywa na  Serikali ya Mtaa kuhakikisha swala hilo linatokomezwa kabisa na mwisho alizungumzia vikao na wanamtaa  vinavyosaidia kutatua tatizo hilo.
 Mmoja wa Mabinti ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa anatoa ushuhuda wa kuachishwa shule,na hapa alipo hasomi na kampeni ya Binti wa kitaa kupitia wadau watafanya jambo kwa Binti huyu
Mwanaharakati Kijana Victoria Mwanziva akijibu swali na kuelezea kwa kina tafsiri ya Jinsia
 Mwezeshaji wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Steven Mfuko akiwahoji baadhi ya Maswali watoto hawa wenye umri wa miaka 12 kama wanajua maswala mbalimbali kuhusu wao na kusema kwamba hawafahamu, na kuomba wapewe elimu juu ya mabadiko yao ya mwili ili kuepuka Mimba za utotoni
 Bi. Mwama Ajabu akielezea namna Simu zilivyoweza kuwaharibu watoto wa kike na kuongeza kuwa wazazi hawana muda nao ndio mana hizo simu zimawaharibu sana, na mara nyingi hufanya mawasiliano kisiri mida ya usiku wakati watu wamelala na kibaya zaidi watoto hao hupendelea zaidi kufatilia mitandao ambayo sio mizuri, ameshauri wazazi mwenzake kuwa lazima wawe karibu na mabinti zao.
 Baadhi ya wahusika wa Binti Kitaa wakiongea na Bodaboda waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa
 Anna akizungumzia Jinsi Binti wa Kitaa inavyofanya kazi
 Hii Timu  ya Binti wa kitaa Wakimsikiliza Mtoto aliyeachishwa Shule na Mzazi wake
 Baadhi ya wahusika wa Binti wa Kitaa wakiwa katika eneo la tukio
 Baadhi ya watu wakiwa katika Mdahalo huo
Mhandisi Eliwanjeria James  kutoka Kikundi cha Mainjinia wanawake Tanzania akielezea kwa kina juu ya kampeni ya Binti wa Kitaa
 Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa  Ambassador Angelo akiendela kutoa Mwongozo


Mwakilishi wa  Sunshine Group akipokea Cheti cha Shukurani kutoka kwa Binti wa Kitaa
Mwakilishi kutoka GW Health World Limited akipokea Cheti cha Shukurani kutoka Binti wa Kitaa
 Bwana Steven Mfuko akitoa Elimu juu ya Mimba za Utotoni na Kuolewa wakiwa chini ya Miaka 18
 Watu mbalimbali wakiwa katika kampeni hiyo
 Kulia ni Binti akitoa ushuhuda wa yeye kupata mimba wakati akiwa na miaka 16 na kusema hiyo ilisababishwa na familia yake
Aliyemwakilisha Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Tabata  Sajenti Geoffrey Kapenejele ambaye pia yupo katika Dawati akielezea namna wanavyotoa elimu kuhusiana na Jinsia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashuleni pia kwa madereva Bodaboda ambao wamekuwa wakilalamikiwa  kusababisha Mimba nyingi za utotoni, Mwisho aliomba jamii kwa ujumla kushirikiana ili kupiga vita swala hilo
Bwana nidhamu wa Madereva wa Bodaboda kituo cha Cecy Bwana Atupele akieleza namna elimu ya maswala ya Jinsia ilivyo wasaidia wao kuunga mkono kupambana na mimba za utotoni ambapo wamejiwekea utaratibu wa adhabu kali kwa yeyote atakayempa mimba binti mwenye umri wa chini ya miaka 18
Mambinti wakiwa katika Kampeni ya Binti wa Kitaa
Mwakilishi wa Sunshine Group Fatuma akielezea namna mimba za utotoni zinavyo athiri maisha ya Binti na pia kusababisha matatizo ya kiafya na kumsababisha akose mambo mengi na kuahidi kuendelea kushirikiana na kampeni ya Binti wa Kitaa kupinga swala hilo
Mwakilishi kutoka TBC FM akielezea majukumu yao ya kuhakikisha kila mtu anapata habari na taarifa pia elimu juu ya kupinga Mimba za utotoni pamoja na ndoa
Bwana Makundi kuroka Radio France RFI akielezea namna baadhi ya Nchi zenye machafuko zinavyo wanyanyasa mabinti wadogo wenye chini ya umri wa miaka 18 kwa kuwaoa, kufanya nao ngono pia kuwahusisha katika mashambulizi mbalimbali, Pia alieleza kuwa vyombo vya Habari vina jukumu kubwa sana la kuhakikisha jamii inapata taarifa na elimu juu ya kupinga mimba na ndoa za utotoni
Kila sehemu ambapo Kampeni ya Binti wa Kitaa inapita huwa panaachwa alama inayo onesha kuwa kuna kitu kilifanyika hapa Meneja wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Mhandisi Eliwanjeria James (kushoto) akiwa na mtoto ambaye aliachishwa shule na Baba yake , hapa anakabidhiwa rasmi kwa wawakilishi wa Sunshine Group Ltd pamoja na GW Health limited kwa ajili ya kusomeshwa ili amalizie masomo yake
Picha ya pamoja 
Picha zote na Fredy Njeje

No comments: