Thursday, November 10, 2016

DC CHUNYA AAGIZA TOZO ZOTE ZA VIJIJI NA MALISASILI KUINGIZWA KATIKA TAARIFA

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa


Na Mwandishi wetu,Chunya

Mkuu wa Wilaya ya Chunya  Rehema Madusa ameitaka halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha kwamba tozo zote za vijiji za Maliasili zinatozwa na zinaonekana kwenye taarifa ya mapato na matumizi.

Aidha ameitaka halmashauri kuingiza  takwimu halisi za
mazao yote yanayo toka katika maeneo ya vijiji husika.

Agizo hilo, amelitoa leo  baada ya kutembelea  na kukagua shughuli za kilimo cha umwagiliaji zinazoendelea katika skimu ya Ifumbo, ambayo serikali imewekeza kiasi cha shilingi milioni 900.

Amesema, licha ya serikali kuwekeza kiasi hicho cha fedha, bado eneo hilo linakabiliwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato kwani asilimia kubwa  ya mapato hayo yamekuwa hayakusanywi ipasavyo kutokana na kukithiri kwa njia za panya.

“Serikali inapoteza fedha nyingi na hii inatokana na kutokuwepo kwa  mfumo bora wa ufutiliaji wa mazao hivyo mchakato huo utasaidia kuongeza mapato katika Wilaya na halmashauri yenyewe,”amesema.

Hata hivyo, amesema nguvu kubwa iliyopo sasa ni kudhibiti njia zote za panya hasa katika eneo la Shoga ambalo ndio eneo linalotumiwa zaidi na wafanyabiashara wasio waaminifu.

Mwisho.

No comments: