Saturday, December 3, 2016

Picha za semina ya Ready to Work ilivyoendeshwa na wasanii wanaowania EATV Awards

Wasanii wanaowania  tunzo za EATVleo walifanya semina na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilikuwapa uthubutu wa kutambua vipaji vyao na kuvifanyia kazi ili kuweza kukabiliana na soko la ajira pindi watakapomaliza masomo yao.


Semina hiyo iliyoendeshwa na benki ya Barclays chini ya pango wake wa ready to Work ilifanyikakatika ukumbi wa Nyerere uliopo katika eneo la Chuo Kikuu Mlimani ambapo jumla ya wasanii 45 waliochaguliwa kuwania tunzo za EATV walihudhuria.

PICHANI JUU: Mwakilishi kutoka Barclays Bank,  Joe Bendera akiongea na wanahabari waliohudhuria seminaya wasanii kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam yenye lengo la kuelimisha wanavyuo kuhusiana na kugundua vipaji vyao na kuvifanyia maamuzi baada ya masomo ilikukwepa adha ya ukwasi wa ajira inayolikabili Taifa
 Hapa ni Kajala Masanja anayewania tunzo ya muigizaji bora wa Kike akiongea na wanahabari
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha dar es Salaam wakisikiliza shuhuda za wasanii mbali mbali wanaowania tunzo za EATV katika semina ya ushawishi wa kugundua vipaji vyao na kuvifanya kazi iitwayo Ready to Work inayosimamiwa na benki ya Barclays
 Mjadala ukiendelea

 Lady Jaydee amble anawania tunes ya msanii Bora wa kike akijibu maswali ya wanafunzi
Mmoja kati ya wasanii wanaowania tunzo ya Msangi Bora wa kiume Daudi Tairo a.k.a Duma akijibu hoja za wanafunzi
 Khadija Ally anayewania tunzo ya muigizaji bora wa kike akiongea wakati wa semina ya Ready to Work inayoshirikisha wasanii wanaowania tunzo za EATV
 Mwakilishi wa Benki ya Barclays akijibu hoja za wanafunzi kuhusiana na mpangowa Ready to Work unaoendeshwa na benki hiyo
 Mwanafunzi akiuliza swali
Kahala Masanja akijibu hoja

No comments: