Wednesday, December 7, 2016

WAZIRI NAPE AJIUNGA NA PSPF, AWASIFU KWA HUDUMA ZA "MWENDO KASI"

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses Nnauye, (wapili kushoto), akipokea fomu ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bw. Adam Mayingu, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Bolggers Tanzania, (TBN), uliomalizika jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa TBN, Bw. Joachim Mushi.
 Waziri Nape, akipokea kadi yake ya kujiunga na Mfuko huo
kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.

NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses Nnauye, amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF na kuusifu kwa huduma zake za haraka.
Waziri Nape, amejiunga muda mfupi baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), kwenye jingo la kitega uchumi la Jubilee Towers linalomilikiwa na Mfuko huo jana.
Aidha washiriki wa mkutano huo nao pia walijiunga na Mfuko huo kupitia uchangiaji wa Hiari yaani PSS.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi yake ya uanachama iliyotengenezwa chini ya dakika 15, Waziri Nape alisema, “Aise, kitambulisho change tayari, hongereni sana kwa huduma za haraka, mimi sikujua kama mnafanya kazi kwa kasi yanamna hii,” alisema Mh. Nape wakati akikabidhiwa kadi hiyo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi ofisini kwake.
Tangu kujaza fomu, kupiga picha na kukabidhiwa kitambulisho hicho, Waziri alitumia kiasi cha dakika 25 tu, ikiwa ni muda mfupi baada ya kufunga mkutano huo.
Nao wanachama wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), waliokuwa wakishiriki mkutano huo, wamejiungana PSPF, baada ya kupatiwa maelezo ya kina kuhusu umuhimu wa kujiunga na Mfuko, kutkana na manufaa mengi ukiachilia mbali kujiwekea akiba.
“Ukiwa Mwanachama wa Mfuko, moja ya faida kubwa ni kujipatia bima ya Afya, itakayokusaidia wewe na familia yako, nikiwa na maana ya mke/mume na watoto,” alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdyul Njaidi katika mada yake aliyoitoa kwa washiriki kuhusu kazi za Mfuko huo.

 Waziri Nape, akijaza fomu hiyo, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu na kulia ni Bw. Njaidi

 Bw. Njaidi akitoa mada kuhusu kazi za Mfuko huo kwa washiriki wa mkutano wa TBN
  Bw. Njaidi akitoa mada kuhusu kazi za Mfuko huo kwa washiriki wa mkutano wa TBN
 Washiriki wa Mkutano wa TBN, wakijaza fomu, huku Bw. Njaidi akitoa maelezo zaidi kwa baadhi yao
 Bw. Mayingu akimkabidhi zawadi Waziri Nape
 Waziri Nape, baadhi ya wafadhili wa mkutano kutoka PSPF, na NMB, wakiwa aktika picha ya pamoja na baadhiya washiriki wa mkutano huo wa TBN
 Mmiliki wa Blogu ya Libeneke la Kaskazini kutoka Arusha Bi. Woinde Shizzah akijaza fomu za kujiunga na PSPF

 Baadhi ya washiriki wakijaza fomu za kujiunga na PSPF




 Waziri Nape akimkabidhi Bw. Seria Tumainieli kadiya kujiungana PSPF
 Waziri akimkabidhi Bi. Veronika kadi ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
  Waziri akimkabidhi Bw. Gadiola Emmanuel kadi ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF

No comments: