Saturday, January 21, 2017

NHIF TANGA YATOA MIKOPO YA VIFAA TIBA NA UKARABATI KWENYE HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa Tanga (NHIF) umefanikiwa kutoa mikopo ya vifaa tiba na ukarabati katika vituo vya afya na hospitali vyenye thamani ya Milioni 559.2.

Vituo ambavyo vilikopeshwa ni Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo, Hospitali za

wilaya ya Korogwe, Lushoto, Handeni ikiwemo vituo vya Afya Makorora, Kituo cha Afya Pongwe, Mikanjuni na Ngamiani.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja wa Mfuko huo mkoani hapa, Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akielezea taarifa ya utendaji kwa waandishi wa habari mjini hapa

Alisema baadhi ya vituo vya afya  vilivyokopeshwa na mfuko huo kati yao vinne vimemaliza kurejesha mikopo yao ambavyo ni Hospitali ya wilaya ya Pangani,Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo (mkopo wa awali) na kituo cha Afya cha Besha na Makorora ambapo ni mkopo wa
awali.

Meneja huyo alisema licha ya kuwepo kwa uhamasishaji mkubwa
wanaoufanya lakini vituo vingi havijachangamkia fursa hiyo ya mikopo ya vifaa tiba, ukarabati wa majengo na dawa.

“Hivyo nivisihi vituo kujitokeza kuchangamkia fursa hii ya mikopo ya vifaa tiba, ukarabati wa majengo na dawa kwenye maeneo yao “Alisema Meneja huyo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments: