Wednesday, January 18, 2017

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yazinduliwa

shinda-nyumba-awamu-ya-pili-1
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho akimkaribisha Mgeni Rasmi, wanahabari na wageni wengine kwenye hafla fupi ya Uzinduzi wa Shindano la Bahati nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili ya Kampuni hiyo.
shinda-nyumba-awamu-ya-pili-2
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe na Kiongozi Mwandamizi wa bodi hiyo, Sadick.
shinda-nyumba-awamu-ya-pili-3
Abdallah Mrisho akitoa maelekezo ya namna ambavyo mshiriki wa shindano hilo anapaswa kufanya. shinda-nyumba-awamu-ya-pili-4
shinda-nyumba-awamu-ya-pili-7Eric Shigongo, akitoa ufafanuzi kuhusu maandalizi maboresho yaliyofanyika kwenye Shinda 
.shinda-nyumba-1
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Saleh Ally akifuatilia kwa karibu uzinduzi huo.shinda-nyumba-2
shinda-nyumba-3
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers, wageni na waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi huo.
shinda-nyumba-awamu-ya-pili-8Mrisho akimkaribisha Bwana Mbalwe.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-9 shinda-nyumba-awamu-ya-pili-10James Mbalwe akizungumza jambo wakati alipozindua Shinda Nyumba Awamu ya Pili ya Global Publishers.
shinda-nyumba-awamu-ya-pili-12 Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe (katikati) akizindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili na kumkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo kipeperushi chenye maelekezo ya namna ya kushiriki.
shinda-nyumba-awamu-ya-pili-11James Mbalwe, akimkabidhi Mrisho kipeperushi. shinda-nyumba-awamu-ya-pili-13....Akimkabidhi kipeperushi Bwana Sadick.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-14James Mbalwe na viongozi wa Global Publishers wakielekea kwa wanahabari kwa ajili ya kuwagawia vipeperushi hivyo. shinda-nyumba-awamu-ya-pili-15 shinda-nyumba-awamu-ya-pili-16 shinda-nyumba-awamu-ya-pili-17James Mbalwe akiendelea kugawa vipeperushi. shinda-nyumba-awamu-ya-pili-18Wanahabari wakifuatilia na kuchukua matukio wakati wa hafla hiyo.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-19Mwanahabari akiuliza swali kwa Meneja, Abdallah Mrisho.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-20
Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel 10, Said Makala akiuliza swali kwa Mkurugenzi, Eric Shigongo.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-21 shinda-nyumba-awamu-ya-pili-22Baada ya kuzindua Shinda Nyumba Awamu ya Pili.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-24
shinda-nyumba-awamu-ya-pili-25Viongozi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Viongozi wa Kampuni ya Global Publishers pamoja na wafanyakazi wake na wanahabari waliofika kwenye uzinduzi huo wakiwa, hapa wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya Lango Kuu la Ofisi za Global Publishers. shinda-nyumba-awamu-ya-pili-26 shinda-nyumba-awamu-ya-pili-27Sebene likiuungurumishwa nje ya lango la ofisi hizo.
DAR ES SALAAM: Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi na Championi, imezinduliwa rasmi leo kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo alisema wameamua kutoa nyumba kama sehemu ya kurudisha wanachokipata kutoka kwa wasomaji na kuwahakikishia kwamba, mchakato mzima huendeshwa kwa umakini, haki na kuzingatia sheria kwa hiyo watu wasiwe na wasiwasi kwamba mshindi atapendelewa.
"Niwahakikishie wasomaji na Watanzania wote kwamba shindano hili lipo 'fair' kabisa na maombi yangu ni kwamba kweli nyumba iende kwa mtu anayeihitaji, kama mjuavyo kujenga nyumba Dar es Salaam ni ghali sana na watu wengi wanapenda kuishi Dar es Salaam.
"Awamu hii tumeyafanyia kazi mapungufu yote yaliyotokea kwenye shinda nyumba iliyopita, nyumba imeboreshwa na ipo karibu na barabara, pia samani zote za ndani zimeboreshwa pamoja na mfumo mzima wa ukusanyaji wa kuponi ambapo utamfikia msomaji karibu zaidi sehemu yoyote alipo nchini," alisema.
Kwa upande wa mgeni rasmi, aliwahakikishia washiriki wote kwamba amekuwa akifanya kazi na Global Publishers na ana uhakika kuwa huwa wanazingatia sheria na ndiyo maana wamewapa kibali cha kuendesha shindano hilo.
"Nimefanya kazi kwa muda mrefu na Global Publishers, huwa hakuna kupanga matokeo wala upendeleo, anayeshinda anakuwa ni yule kweli aliyestahili, nawasihi watu wote washiriki kwa sababu shindano limefuata taratibu zote za kisheria," alisema.
Kwa upande wa Meneja Mkuu wa Global Publishers, aliwataka watu wengi washiriki kwa sababu yeyote anaweza kuibuka mshindi na kueleza kuwa namna ya kushiriki kuwania nyuumba hiyo iliyopo Bunju, Dar, mshiriki anatakiwa kununua magazeti la Global Publishers, kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili na kuijaza kisha kuikusanya kwa wakala aliye karibu naye nchi nzima au kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge jijini Dar.
Picha na Richard Bukos na Amani Madebe/GPL
shinda-nyumba-ii

No comments: