Tuesday, March 28, 2017

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA JUMUIYA YA WANAWAKE WALIOJIAJIRI (SEWA) KUTOKA INDIA

Mh Makamu wa Rais akipokea taarifa ya ziara kutoka kwa Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala pamoja na Pushpa Rathod - SEWA Makamu wa Rais baada ya kuvishwa alama ya heshima kwa mila za Kihindi kutoka kwa Pushpa
Rathod “Deputy High Commissioner” India Bw. Robert Shetkintong,wa pili kutoka kulia mwenye suti katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassa, Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala, Pushpa Rathod , Sophia Kinega kiongozi wa wanawake waliojiajiri na Mhe. Siriel Mchembe msaidizi wa Mama Samia kwenye jopo la juu la dunia katika kuwezesha wanawake kiuchumi amekubali kuanzisha Jumuiya hiyo hapa Tanzania. SEWA – “Self Employed Women Association” ni Jumuiya ya Wanawake Waliojiajiri ambayo miongoni mwa viongozi wake wakuu ni Bi. Renana Jhabvala (Chair Women in Informal Employment WIEGO. Aidha, Bi Renana na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais JMT ni miongoni mwa viongozi wakuu wa Jopo la Juu Duniani katika Kuwezesha Wanawake Kiuchumi chini ya Umoja wa Mataifa. Ushirikiano wa viongozi hawa unandelea kuleta mafanikio makubwa kwa Wanawake hasa wa ngazi ya chini hapa Tanzania. Baada ya ujumbe huo kutua Tanzania tangu tarehe 21 – 26 Machi, 2017, wanawake wa Zanzibar na Tanzania Bara wamepata mafunzo mbalimbali kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali. Taasisi zilizoshiriki ni TEWO SACCOS, JUWABIKA, UWAKE, BACCA, BAMITA na MKUDUWODEA. Mhe. Makamu wa Rais baada ya kukutana na ujumbe huo tarehe 27/3/2017 ukioongozwa na “Deputy High Commissioner” India Bw. Robert Shetkintong, akiongozana na Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala, Pushpa Rathod , Sophia Kinega kiongozi wa wanawake waliojiajiri na Mhe. Siriel Mchembe msaidizi wa Mama Samia kwenye jopo la juu la dunia katika kuwezesha wanawake kiuchumi amekubali kuanzisha Jumuiya hiyo hapa Tanzania. Mchakato wa kuanzisha Jumuiya ya wanawake waliojiajiri India na Tanzania (SEWA) unaanza mara moja chini ya ulezi wake.Wanawake waliojiajiri Tanzania hongereni kwa kupata sauti Duniani.

No comments: