Monday, June 21, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Lina wa THT Azua kichekesho cha World Cup
Soka ina wenyewe, kwahiyo comment kuhusu World Cup ziachwe kwa watu wenye uelewa na mchezo husika, vinginevyo ni kichekesho.

Mtoto mzuri anaye-shine kupitia mradi wa Tanzania House of Talent (THT), Lina wiki iliyopita aliacha kichekesho, alipotakiwa na Watangazaji wa Clouds TV kutoa maoni yake kuhusu michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Lina alisema kuwa kuhusu michuano ya World Cup inayoendelea huko Afrika Kusini jicho lake analitupia kwenye timu ya Real Madrid kwa sababu anampenda sana mchezaji Cristiano Rodaldo.

Hicho ni kituko kwa sababu Real Madrid ni klabu kwahiyo haishiriki michuano ya Kombe la Dunia ambayo inashirikisha mataifa tu! Hata Ronaldo anayemsema, amekwenda Afrika Kusini na timu yake ya taifa ya Ureno. Ni suala la kujifunza tu!
*******************************
John Legend Aparamia kitandani na kuwachakachua warembo sita, atinga Bongo na wa ukweli
Mpango ule ule wa nani kavurugana na yupi in bed unachukua nafasi yake, staa wa R&B nchini Marekani, John Legend anaingia kwenye bwawa la viulizo na anachambuliwa kama ifuatavyo:

Kwa mujibu wa mtandao unaodili na ishu za nani kadondoka kwa nani na kwa staili ipi, Jessica White ndiye mnyange anayetajwa wa kwanza kwenye orodha, ikiwekwa wazi kwamba walichakachuana mwaka 2005. Akaja Wafah Dufour, akaunga Danielle Abreu, akafuata Tayo Otiti ambapo wote hao watatu walikubali kuanguka naye dhambini mwaka 2006.

Mrembo Christy Teigen ambaye ndiye ‘wa ukweli’ alianza naye mwaka 2007 na kinaeleweka hadi sasa lakini kati ya 2007-2008, Legend alimsaliti mchumba wake na kuchangamsha damu na mtoto mzuri, Petra Nemcova.

...atua Bongo na wa ‘ukweli’ Christ Teigen
Character wa Abby Cool & MC George over the weekend pande za Tabora, Juma Kapipi anaripoti kuwa wiki iliyopita, John Legend akiwa na mchumba wake, mwanamitindo Christine Teigen ‘Christy’, walitinga Bongo na moja kwa moja wakatia maguu mpaka kwenye vijiji vya Millennia Mbola vilivyopo Wilaya ya Uyui. Legend, alitinga Mboka kimya kimya na kutembelea vijiji hivyo ili kujionea miradi ya maendeleo ambayo mwanamuziki huyo ni mmoja wa wafadhili.

Mwanamuziki huyo anafadhili miradi ya maendeleo kwenye Vijiji vya Millennia Mbola, Tabora kupitia mradi wake wa The Show Me Campaign. Legend, alitinga Tabora akitokea Afrika Kusini ambako alihudhuria sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia mwaka 2010, zilizochukua nafasi Juni 11 kwenye Uwanja wa Soccer City, Johannesburg.

Mkali huyo kutoka Marekani, ni mmoja wa wanamuziki ambao walialikwa kutumbuiza kwenye sherehe za awali za ufunguzi. Baada ya kutinga Tabora, mwanamuziki huyo aliridhishwa na utekelezaji wa mradi huo wa Vijiji vya Millennia Mbola ambao lengo lake ni kupunguza umaskini kwa wananchi.

Akiwa kwenye Vijiji vya Millennia Mbola, Legend aliahidi kuendelea kuwahamasisha wafadhili mbalimbali duniani kuchangia mradi huo. Legend pia aliwaimbia nyimbo mbili wakazi wa vijiji hivyo ambazo maudhui yake ilikuwa ni kuwataka kuungana pamoja katika kutokomeza umaskini.

Siku mbili zilitosha kukamilisha ziara yake na kurudi nchini kwake, Marekani. Jina lake kamili John Stephens na Legend ni a.k.a. Alizaliwa Desemba 28, 1978, Ohio, Marekani. Ni mshindi mara sita wa Grammy Awards, mwaka 2007 alitunukiwa tuzo maalum ya Starlight kutoka Songwriters Hall of Fame.

Amewahi kufanya kazi na wakali kama Kanye West, Slum Village katika ngoma “Selfish”, Dilated Peoples’ “This Way”, Jay-Z “Encore”, aligonga backing vocals katika wimbo wa Alicia Keys “You Don’t Know My Name” na Fort Minor “High Road.” Alipiga piano kwa Lauryn Hill kwenye track “Everything Is Everything”.
************************
Diamond Musica Yateka soko la burudani Bongo!
Kutesa kwa zamu! Imezungumzwa hivyo na inaonekana mambo kwenda mswano kwa Bendi ya Diamond Musica International ‘Vijana Classic’, kwani kwa sasa ndiyo inayoonekana kuteka soko la muziki wa dansi nchini. Tathmini ambayo imefanywa na Abby Cool & MC George over the weekend, imeonesha kwamba Diamond Classic ambao a.k.a yao nyingine ni ma-Handsome wa Jiji ndiyo bendi inayopiga shoo nyingi Tanzania Bara hasa katika kipindi hiki.

Safu hii imebaini kuwa ubora wa nyimbo za Diamond Musica, shoo ya kiwango cha juu inayodondoshwa na timu nzima kuanzia wanenguaji hadi waimbaji, utanashati wao na mapigo bomba ya muziki, ni pointi zinazosababisha bendi hiyo kugeuka watawala wa dansi.

Kazi nzuri ya Mkurugenzi Mtendaji, Judith Moshi na bosi mwingine wa bendi hiyo, Perfect Kagisa ‘P Diddy’ ya kumnyakua mwimbaji na mtunzi wa kiwango cha juu, Mulezili Boyange ‘Mulemule FBI’ pamoja na kuboresha safu ya upigaji vyombo, uimbaji na unenguaji ni sababu ya Diamond kung’ara kwa sasa.

FBI ambaye kwa sasa ndiye Rais wa bendi, Makamu wa Rais Yanick Noah ‘Sauti ya Radi’, mkali Alarn Mulumba Kashama, Patrick Simpuka ‘Juisi ya Machungwa’, Mugogo ya Mazizini na wengineo wapya kwa pamoja wameifanya Diamond izifunike bendi nyingine ambazo zilikuwa zimekwishajionesha kama watawala wa muziki.

Safu hii ina maelezo kwamba katika kipindi hiki ambacho mashindano mengi ya urembo yanafanyika kuelekea Miss Tanzania, Diamond ndiyo bendi ambayo imepiga shoo nyingi mikoani kusindikiza maonesho mbalimbali.

Safu hii inatoa Big up kwa Diamond Musica, bila shaka kasi yenu inafaa kuwa mfano wa kuigwa na bendi nyingine nchini, kwani nyingi zimetuama Dar wakati nyinyi mnavuma nchi nzima.
************************
Compiled by mc george/ijumaa wikienda

4 comments:

Anonymous said...

E bwana Mrisho vp mbona mtandao wa Global haupatikani au mmebadilisha address,nimemiss kweli hadith.
mdau UK.

Mrisho's Photography said...

Hellow..naomba unisaidie, mtandao wetu haupatikani kivipi..mbona hauna matatizo yoyote? Naomba nitumie unapata msg gani unapoufungua? anuani yetu bado ni ile ile www.globalpublishretz.com au just search google global publishers tanzania na utaona anuani kibao ikiwemo ya globalpublishers.info...yoyote utakayoichagua itakufikisha GPL.....fanya hivyo kisha nijulishe ndugu...

Anonymous said...

Hellow tena ndugu yangu Mrisho nimejaribu kufanya hivyo inakuwa inaniletea msg ya Firefox can't find the server at www.globalpublishers.info.
sasa sijui kwa sababu natumia Firefox ila toka mwanzo nilikuwa natumia hii Firefox.

Bablee said...

Mkuu last week nlikwambia haipatikani ukanichunia, but kiikweli mimi binafsi huwa naingia global kwa ku click hiyo link uloonesha hapo (Favorite websites) Lakini naambulia maumivu tu.