Friday, June 18, 2010

IJUMAA SHOWBIZ

Nas Damian Marley: Watupia Kiswahili kwenye ngoma yao
Katika kile kinachoonesha kwamba Lugha yetu ya Taifa a.k.a Kiswahili inaendelea kupasua anga ulimwenguni, mastaa wawili wa muziki wa Hip Hop Marekani, Nas Escoba na mtoto wa Hayati Bob Marley, Damian Marley wameitupia lugha hiyo kwenye ngoma yao yenye jina la As We Enter.

Washkaji hao ambao wamesimama vyema kwenye kolabo hiyo ya ukweli ambayo wameimba kwa kupokezana wametumia maneno ya kiswahili kama “Habari gani”, “Nzuri sana” na kuifanya lugha yetu kutambulika na mataifa mbalimbali duniani. Zaidi icheki ngoma hiyo hapo chini huku maneno ya kiswahili yakiwa yamewekewa rangi ya nyekundu.
Nas & Damian Marley As We Enter lyrics

[Damian Marley]
As we enter
Come now we take you on the biggest adventure

[Nas]
Must be dementia, that you ever thought
You could touch our credentials, what's the initials?

[Damian Marley]
You be Jamrock the lyrical official
Send out the order, laws and the rituals

[Nas]
Burn candles, say prayers, paint murals
It is truth we big news, we hood heroes

[Damian Marley]
Break past the anchor, we come to conquer
Man a badman, we no play Willy Wonka

[Nas]
And I got the guns

[Damian Marley]
I got the ganja

[Nas]
And we could blaze it up on your block if you want to
Or haze it up stash box in a Hummer
Or you could run up and get done up

[Damian Marley]
Or get something that you want none of
Unlimited amount you collect from us
Direct from us, street intellectuals

[Nas]
And I'm shrewd about decimals
And my man'll speak Patois
And I can speak rap star
Y'all feel me even if it's in Swahili
Or body Ghani (Habari Gani)

[Damian Marley]
Masuri Sana (Mzuri Sana)
Switch up the language and move to Ghana

[Nas]
Salute and honor, real revolution rhymers

[Damian Marley]
Rhythm piranhas

[Nas]
Like true Obamas, unfold the drama

[Nas]
Word is out, hysteria you heard about
Nas and Jr. Gong gonna turn it out
Body the verse until they scream "murder" out
The kings is back, time to return the crown
Who want it? Tuck your chain, we're due coming
Renegades that'll peel you back like new hundreds
Bet your jewels on it, you don't want to lose on it
Either move on or move on it

[Damian Marley]
Queens to Kingston
Gunshot we use and govern the kingdom

Rise of the Winston, I can see the fear up in your eyes
Realize you can die any instant

[Damian Marley]
And I can hear the sound of a voice
When you must lose your life like mice in the kitchen

[Nas]
Snitching, I can see him pissing on hisself
And he's wetting up his thighs and he trying to resist it

[Damian Marley]
Switching, I can smell him digging up shit like a fly
Come around and be persistent

[Nas]
That's how you end up in a hitlist

[Damian Marley]
Ain't no bad man business

[Nas]
No evidence

[Damian Marley]
Crime scene, fingerprint-less

[Nas]
Flow effortless

[Damian Marley]
Casual like the weekends

[Nas]
No pressure when

[Damian Marley]
We're comfy and decent

[Nas]
We set this off beasting

[Damian Marley]
Hunting season

[Nas]
And, frankly speaking...
Word is out, hysteria you heard about
Nas and Jr. Gong gonna turn it out
Body the verse until they scream "murder" out
The kings is back, time to return the crown
Who want it? Tuck your chain, we're due coming
Renegades that'll peel you back like new hundreds
Bet your jewels on it, you don't want to lose on it
Either move on or move on it
Word is out, hysteria you heard about
Nas and Jr. Gong gonna turn it out
Body the verse until they scream "murder" out
The kings is back, time to return the crown
Who want it? Tuck your chain, we're due coming
Renegades that'll peel you back like new hundreds
Bet your jewels on it, you don't want to lose on it
Either move on or move on it
***********************************************

Dk. Cheni
Sajuki
Dk Cheni: Awatosa Wadosi kusimamia One By One
Kutoka ndani ya tasnia ya muvi Bongo, staa wa game hiyo Mahsein Awadh ambaye hivi karibuni anatarajia kudondosha kitaani filamu yake mpya, One By One amesema na ShowBiz kwamba kila kitu kuhusu mzigo huo atasimamia mwenyewe.

“Unajua mara nyingi sisi Wabongo huwa tunaogopa kujaribu, mimi nimejitoa muhanga kusimamia kazi zangu mwenyewe kuanzia maandalizi mpaka sokoni badala ya kuwapelekea Wahindi. Nataka nione faida na hasara ili nijue wapi nimekosea ili nijipange vizuri,” alisema Dk Cheni.

Muvi hiyo, One By One ambayo hivi karibuni ilitambulishwa kwa wadau wa filamu kabla ya kuingia sokoni ipo katika maudhui ya kutisha tofauti na kazi nyingine alizowahi kupiga msanii huyo. Baadhi ya wasanii wengine aliowapa shavu ni pamoja na Dotnata na mumewe, Posh, Sajuki na wengine.
******************************************************
Kolabo kwenye Gospel vipi?- Braton
Kutoka pande za Magomeni, Dar prodyuza na msanii wa muziki wa kizazi kipya Braton Mbwana a.k.a Braton amesema na ShowBiz kwamba bado hajui kwanini wasanii wa muziki wa Injili Bongo hawana ushirikiano katika nyimbo zao.

Akipiga stori na safu hii juzi, Braton ambaye kupitia studio zake za Backyard ametoa nafasi kwa wanamuziki kurekodi bure nyimbo za kuelimisha jamii kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu, alisema kwamba. “Tofauti na ilivyo kwa wenzetu hasa wa Marekani huwa wanashirikiana na kufanya kazi nzuri, wakiwemo kina dada wa kundi la Mary Mary ambao wamempa shavu Kirk Frankline katika wimbo wao, Thank You.

“Kwa hapa kwetu Bongo nimewahi kusikia kolabo moja tu ambayo Bony Mwaitege alifanya na Bahati Bukuku katika wimbo wa Utanitambuaje ambao kiukweli una mvuto hadi hii leo. Nawashauri wafanye hivyo kama ilivyo sisi kwenye muziki wa kizazi kipya ili walete radha tofauti katika nyimbo hizo za kuabudu.
****************************************************

Twanga Na historia ya Kisa cha mpemba
Bendi ya African Stars a.k.a Twanga Pepeta ambayo iko tayari kuadhimisha miaka kumi tangu kaanzishwa kwake imejipanga sawasawa kuwakumbushia mashabiki wake ngoma za kitambo ikiwemo Kisa cha Mpemba ambayo ni albamu yao ya kwanza.

Akipiga stori na safu hii juzi kati, Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka alisema kwamba mbali na Kisa cha mpemba albamu zote kumi walizowahi kutoa zitakumbukwa bila kusahau tuzo walizowahi kupata na mafanikio mengine ya bendi hiyo maarufu.

“Albamu kumi tulizowahi kutoa ni Kisa cha mpemba (2000), Jirani (2001), Fainali uzeeni (2002), Chuki Binafsi (2003), Ukubwa jiwe (2004), Safari (2005), Mtu pesa (2006), Password (2007), Mtaa wa kwanza (2008) na Mwana Dar es Salaam (2009).

“Shughuli nzima itafanyika ndani ya Viwanja vya Leaders Club Juni 27, mwaka huu kwa maandamano yatakayoanzia katika ofisi zetu za ASET zilizopo Kinondoni na kuishia katika viwanja hivyo ambapo zitafanyika burudani mbalimbali kabla vijana wa Twanga hawajapanda jukwaani,” alisema Asha Baraka.
compiled by mc george/ijumaa newspaper

2 comments:

Anonymous said...

Samahani ndugu yangu mbona siwapati global publisherzz tangu iki iliyopita

Anonymous said...

Vp mkuu mbona mtandao wa Globalpublisher haupo hewani kulikoni?