Friday, June 2, 2017

MKURUGENZI MANISPAA YA UBUNGO NDG JOHN L. KAYOMBO AKABIDHIWA JEZI NA BENKI YA NMB KWA AJILI YA MICHEZO YA UMITASHUMTA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizikagua jezi alizokabidhiwa na  Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine Mushi wakati wa dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo uliopo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Baadhi ya washiriki wakifatilia kwa karibu dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo uliopo Mtaa wa Kibamba ChamaJijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa  
makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya UMITASHUMTA dhifa iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo uliopo Mtaa wa Kibamba Chama
Meneja Mahusiano Biashara za serikali Bi Mkunde Joseph kutoka Benki ya NMB Makao Makuu akielezea dhamira ya kuchangia vifaa hivyo vya michezo kwa ajili ya wanafunzi wanaoshiriki UMITASHUMTA wakiwakilisha Manispaa ya Ubungo

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine Mushi akielezea dhamira ya kuchangia vifaa hivyo vya michezo kwa ajili ya wanafunzi wanaoshiriki UMITASHUMTA wakiwakilisha Manispaa ya Ubungo, (Kulia) ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau kutoka Benki ya NMB sambamba na watumishi wa Manispaa ya Ubungo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine Mushi wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine Mushi wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau kutoka Benki ya NMB sambamba na watumishi wa Manispaa ya Ubungo

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo leo June 2, 2017 amekabidhiwa na Benki ya NMB jezi seti tatu kwa ajili ya wanafunzi wa Manispaa ya Ubungo.

Jezi hizo zimekabidhiwa kwa Mkurugenzi Kayombo kwa ajili ya maandalizi kwa wanafunzi wanaotaraji kushiriki katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA).

Mashindano hayo yanataraji kuanza kurindima June 16, 2017 katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kuwakutanisha wanafunzi mbalimbali kutoka kote nchini Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa jezi hizo katika dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Ubungo, Mkurugenzi Kayombo ameipongeza Bank ya NMB (National Microfinance Bank PLC (NMB) kwa kutoa jezi hizo kwani Michezo ni moja ya maeneo yanayotumika kutambulisha, kutangaza, kuipatia sifa nchi na hata utajiri kwa wanamichezo wake.

Alisema kuwa Uendelevu wa michezo huwezekana tu kwa kuenzi mfumo wa kutambua vipaji kutoka ngazi za chini, kuviibua na kuvikuza hivyo Benki hiyo kuchangia vifaa hivyo ni dhamira njema katika kuwaunganisha wanafunzi pamoja na kurahisisha utambuzi wa vipaji vyao.

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Njia za makuzi ya watoto zaidi ya nyumbani na katika jamii zao ni pamoja na elimu rasmi shuleni, ambapo Tanzania kwa miaka mingi imeweka pia sera ya kutenga muda wa michezo na taaluma nyingine muhimu kama hii katika shule za msingi.

Alisema Moja ya sifa kuwa za michezo hii, ni kule kushirikisha hata wanafunzi wenye ulemavu, ambao katika baadhi ya maeneo na timu mitaani wamekuwa wakikosa nafasi, licha ya kuwa na kipaji na kuwa na uwezo wa kufanya vyema kuliko wasio na ulemavu.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine Mushi alisema kuwa UMITASHUMTA kwa miaka mingi imekuwa ikidhaminiwa na serikali peke yake, na uzoefu umeonyesha wazi kwamba wadau zaidi wanapojitokeza kuchangia nguvu katika michezo, mafanikio makubwa hupatikana hivyo kuamua kuchangia ni dhamira njema ya kuunga mkono dhamira ya dhati ya kuanzishwa kwa mashindano hayo.

Bi Evelyine alisema kuwa wachezaji wanaotamba kwenye michezo mbalimbali katika ngazi za juu walianzia chini, na laiti vipaji vyao visingetambuliwa na kukuzwa kwa njia moja au nyingine, ni wazi wsingefikia mafanikio yao.

"Benki ya NMB kuchangia jezi Huko ndiko kuinua michezo, huko ndiko kulijenga Taifa Tanzania katika jukwaa la kimataifa, na ni tangazo tosha kwa utajiri wake wa maliasili" Alisema Bi Evelyine

UMITASHUMTA huendeshwa kwa mfumo wa Kanda, ambapo wanafunzi huchujana kuanzia ngazi za Shule, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa hadi Kanda na kupata timu ambayo husafiri kuchuana na wenzao katika Mji na Mkoa uliopangwa. Kwa kuwa ni vigumu kuibua na kukuza vipaji mitaani katika kila kona ya Tanzania, UMITASHUMTA ni chemchemi bora ya vipaji vya michezo na taaluma, maana ni mkusanyiko wa waliofanya vizuri tangu ngazi ya chini hadi Kanda

No comments: