Friday, September 12, 2008

ZAIN YAONESHA NJIA!

Mwanabloga maarufu na mwanzilishi hapa nchini, Muhidini Michuzi (kulia) akiwa na mwanamuziki maarufu nchini tanzania, Lady jaydee, mara baada ya kutangazwa kuwa mabalozi wa Zain nchini.
Meneja Masoko wa Zain, Constatine Magavila (kati) akiwa na mabalozi wake wakati akiongea na media leo katika makao makuu ya Zain pale Kijitonyama. Zain imekuwa kamouni ya kwanza nchini kuthamini Blogs kwa mchango wake wa kuelimisha na kutoa taarifa kwa haraka.

Zain Yateua Mabalozi wa ‘One Network’

Dar es Salaam, September 12, 2008; Zain kampuni ya simu za mkononi inayoongoza katika nchi 22 Barani Afrika na Mashariki ya Kati imeteua na kutangaza mabalozi wa huduma yake ya One Network, ambayo ni huduma ya kwanza duniani kuondoa mipaka katika mawasiliano.
Zain iliweka historia katika sekta ya wawasiliano duniani ilipozindua huduma ya One Network kwa mara ya kwanza November 2006 ikitoa huduma katika nchi za Afrika Mashariki; Tanzania, Kenya na Uganda. Huduma hii sasa inapatikana katika nchi 16 katika Bara la Afrika na Mashariki ya Kati.
Katika mkutano na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Costantine Magavilla aliwatangaza mwanamuziki maarufu nchini Judith Wambura, anayefahamika kama Lady Jay Dee na Muhidin Issa Michuzi, mwandishi wa habari na mpiga picha mwandamizi kama mabalozi wa huduma ya Zain ya One Network kuanzia Ijumaa mwezi huu.
Lady Jaydee na Michuzi wameteuliwa kwa ajili ya mafanikio waliyonayo katika fani zao. Lady Jay Dee amekuwa katika fani ya muziki kwa kipindi cha miaka saba sasa na ni moja katika ya waimbaji wa kike wanaoongoza nchini kwa sasa. Lady Jaydee ambaye ameajiri watu 10 katika bendi yake, anatajwa kuwa msanii anayeongoza nchini kwa kushinda tuzo nyingi.
Aidha, Lady JayDee ameshinda Tuzo la Shirika la Utangazaji la BBC kwa kuwa na wimbo bora na ametumbuiza mara tatu mbele ya Rais Jakaya Kikwete. Lady JayDee ameteuliwa mara nne kushiriki katika Tuzo za Kora ambapo na mwaka huu atashiriki, vile vile Lady Jaydee ameshinda mara tatu Tuzo Bora ya muziki wa video inayotolewa na Channel O.
Michuzi kwa upande wake licha ya kuwa mwandishi wa habari na mpiga picha mwandamizi mwenye mafanikio pia amamiliki blog ambayo inaoongoza kwa umaarufu nchini ikisomwa na mamilioni ya watu wanaoishi ndani na nje ya Tanzania.
‘’Tunaamini kwa kushirikiana na Lady Jay Dee na Michuzi tutaweza kuwasisimua na kuwafikia watu wengi zaidi na kusambaza habari za huduma yetu kabambe ya One Network inayofanikisha upatikanaji wa mawasiliano kwa urahisi na bei nafuu katika nchi 16, mambo ambayo yatasaidia jamii na uchumi kukua kwa kasi zaidi. Watu wataweza kuendelea kuwasiliana hata wakivuka mipaka, na biashara inayovuka mabara itashamiri zaidi kwa sababu ya huduma yetu ya One Network, ambayo kimsingi ni sehemu ya ahadi ya Zain ya kutengeneza ulimwengu maridhawa.
“Naona fahari kuteuliwa na Zain Tanzania kuwa Balozi wake wa huduma yao ya One Network, na nawashukuru Zain kwa kunifanya sehemu ya huduma hii inayosisimua ya One Network ambayo imebadilisha mawasiliano ya simu za mkononi duniani kwa kuwa huduma ya kwanza kuunganisha mabara duniani kwa kuondoa mipaka na kupunguza gharama za mawasiliano.


‘’Kama Mtanzania siku zote nafurahia kupata fursa ya kufanya jambo linalogusa jamii na katika suala hili ninaona fahari kupewa fursa ya kusambaza habari na mambo mazuri ya manufaa ya One Network ili kuongeza uelewa wa Huduma ya One Network ambayo itafanya mawasiliano wakati wakuvuka mipaka kuwa rahisi na ya gharama nafuu,’’ alisema Lay Jaydee.
Muhidin Issa Michuzi kwa upande wake amesema anaona fahari kuteuliwa na Zain kuwa Balozi wa One Network kuwasaidia kusambaza manufaa ya kibiashara na ya mtu binafsi yanayopatikana kutokana na huduma ya One Network.
“Zain ni kampuni inayosisimua na ninaona furaha kujihusisha na kampuni inayoongoza na kuweza kutangaza manufaa ya kibiashara na ya mtu binafsi yanayopatikana kutokana na huduma ya One Network.

"Kubwa zaidi natoa shukrani kwa Zain kwa kuutambua mchango wa wanahabari hususan blogu na hii heshima si yangu mimi pekee bali ni ya ma-blogger wote wa Tanzania ambao Zain imeanzisha mchakato tunaogombania - wa kutambuliwa rasmi kwamba blogu ni kipasha habari chenye hadhi kama vingine vyote," alisema Michuzi.

Zain mapema wiki hii mjini London imeshinda tuzo ya Dunia ya Miundombinu Bora ya Biashara isiyotumia nyanya kwa sababu ya huduma yake ya ‘One Network’.


Huduma ya One Network inaunganishwa kwenye simu ya mteja wa Zain mara moja mteja akivuka mipaka bila kuwa na urasimu wa kujisajili kabla au kulipia ada ya kujisajili.

Wateja kadhalika wanaweza kupiga na kupokea simu kwa gharama za nyumbani wanapokuwa wanawasiliana na mteja wa Zain aliyesafarini. Mteja huyu naye kwa kutumia One Network atapokea simu zinazoingia bure na ataweza kupiga simu nyumbani kwa gharama za nyumbani.

One Network ni huduma ya kwanza duniani inayoondoa mipaka na kupunguza gharama za mawasiliano kwa kuwawezesha wateja kupiga na kupokea simu bure bila kulipia gharama za zuru za kimataifa wanapovuka mipaka katika nchi 16 ambazo zimeunganishwa na huduma ya One Network Barani Afrika na Mashariki ya Kati.

Wateja pia wataweza kuongeza salio kwa kutumia muda wa maongezezi unaopatikana katika vituo zaidi ya maelfu, vinavyopatikana katika nchi yoyote yenye huduma ya One Network.

‘’Zain inaamini huduma ya One Network itawavutia wateja wengi wapya kwenye mtandao wa Zain, na kadri huduma hii inavyoendelea kukua itachangia kwa kiasi kikubwa kwa Zain kutimiza malengo yake ya mwaka 2011 ya kufikia wateja milioni 150 na kuwa moja kati ya kampuni 10 zinazoongoza duniani kwa mawasiliano ya simu za mkononi,’’ alisema Magavilla.

Nchi zenye huduma ya One Network ni; Bahrain, Burkina Faso, Chad, the Republic of Congo, the Democratic Republic of Congo, Gabon, Iraq, Jordan, Kenya, Malawi, Niger, Nigeria, Saudi Arabia, Sudan, Tanzania na Uganda.

No comments: