Baada ya kurejea nchini kutoka Marekani ambako alikaa kwa wiki kadhaa na kuzua mjadala wa kile kilichotekea huko, mkali wa filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba, aenda Uingereza. Akiongea nami kuhusu safari yake, Kanumba alisema anakwenda London kwa kazi za kisanii na atakuwa huko kwa muda wa wiki tatu hadi nne, kutegemeana na program yake itakavyokwenda.
Aidha hivi sasa ameacha amezindua mtandao wake wa www.kanumba.com ukiwa na lengo la kujitanua kisanii na kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia. Ingawa kwa sasa mtandao huo unaelemewa na watazamaji, lakini mafundi wake wako mbioni kuongeza 'bandwidth' ili kuondoa tatizo la msongamano.

3 comments:
Mbona web yako kanumba haifunguki?sasa kwa nn umeitangaza.Unaboa
ni kweli, mdebwedo web, siku nzima nahangahika, hakuna kitu, kama bado unaiweka ya nni kutupotezea muda.. badala ya kupoteza muda kwa kaka Michuzi....
kwa raha zako mdogo wangu.kutembea ni kuzuri unapata kupanua mawazo na kuongeza ujuzi zaidi big up mjomba .
Post a Comment