Wednesday, August 16, 2017

UVCCM YAWATAKA WAHANDISI ZANZIBAR KUJENGA BARABARA ZENYE UBORA

Meneja Mradi wa Barabara yenye urefu wa km 35  ya Ole Ngeneja Mhandisi Amin Khalid Abdallah akitoa ufafanuzi juu ya maendeleo ya mradi huo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) alipokwenda kukagua ujenzi wa barabara hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba. (Picha zote na Fahad Siraji)
Daktari dhamana katika hospitali ya Chakechake Dkt.Ali Habib Ali akimpokea Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka
(MNEC) alipowasili hospitalini hapo kuangalia wagonjwa na kuwafariji wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akimpatia baadhi ya vifaa tiba Bi, Salha Issa Nassor alipotembelea katika wodi ya kina mama waliojifungua alipowatembelea wagonjwa na kuwafariji katika Hospitali ya Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) (kulia)) akiwasili katika ukumbi wa mkutano Tawi la CCM Wawi kuzungumza na Vijana wa CCM wilayani ChakeChake Mkoa wa Kusini Pemba.
 Vijana wakifuatilia mkutano huo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Vijana wa CCM wilayani ChakeChake Mkoa wa Kusini Pemba katika ukumbi wa mkutano Tawi la CCM Wawi, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  wakati akizungumza na maafisa Wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani, katika ukumbi wa skuli ya Chekechea Mdungu Wilayani ChakeChake Mkoa wa Kusini pemba.
Maafisa wadhamini wa mabaraza ya Mji na Madiwani wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.


Na Mathias Canal, Kusini Pemba

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umekemea baadhi ya wahandisi wasiowajibika ipasavyo kwa kujenga barabara chini ya kiwango ilihali serikali imewalipa fedha zao kadri ya makubaliano.

UVCCM imesema kuwa serikali inapaswa kuwachukulia hatua za kisheria wahandisi wa kariba hiyo ikiwemo kuwanyima tenda sambamba na kuwafikisha mahakani kwani wanaisababishia hasara kubwa serikali kwa kufanya marekebisho ya barabara mara kwa mara.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 15, 2017 alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya Ole-Vitongoji na Mfukiwa-Kengei wakati wa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Unguja.

Barabara hiyo yenye jumla ya urefu wa Kilomita 35 inatarajiwa kukamilika katika hatua za awali mwishoni mwa mwezi Agosti 2017 huku ukamilisho wote ukitaraji kufika ukomo Disemba 2018.

Shaka amepongeza namna barabara hiyo inavyojengwa kwa viwango ambayo itakuwa na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu pasina kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara kama ambavyo baadhi ya barabara zimekuwa zikiharibika na kufanyiwa marekebisho jambo ambalo linaiingizia serikali hasara.

Hadi kufika hatua ya ukamilisho barabara hiyo itagharimu Dola za kimarekani shilingi Milioni 11 ambazo ni sawa na zaidi ya Bilioni 24.4

Hakuna serikali popote duniani yenye uwezo wa kuajiri  vijana wote nchini badala yake serikali nyingi zinafanya kazi ya kuweka miundo msingi ya wananchi kuweza kujiajiri.

Barabara hiyo inajengwa na Wizara ya Ujenzi na utunzaji wa barabara Zanzibar upande wa Pemba kupitia ufadhili wa Mfuko wan chi zinazotoa mafuta kwa wingi Duniani (OPEC).

Naye Meneja Mradi wa barabara hiyo Mhandisi Amin Halid Abdallah amempongeza Kaimu katibu mkuu UVCCM kwa kuzuru katika eneo hilo kujionea hali ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM huku akiahidi kusimamia ujenzi huo kwa weledi na hatimaye kuwa na barabara imara.

MWISHO.

No comments: