Tuesday, August 8, 2017

WATANZANIA WAJITOKEZA KUMSAIDIA JINI KABULA

Msanii wa filamu nchini, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.[/caption] MUDA mfupi baada channel ya mtandaoni ya Global TV Online kuendesha kampeni maalum yakumchangia fedha za kusaidia matibabu na huduma kwa msanii wa filamu nchini, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’,wadau mbalimbali wameonekana kuiunga mkono kampeni hiyo. Kampeni hiyo iliyopewa jina la Support Treatment For Jini Kabula, imeonekana kuwagusa watu mbalimbali hivyo kuahidi kujitolea kwa moyo japo kwa kidogo chochote kadiri watakavyojaaliwa. Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ enzi akiwa salama.[/caption] Kwa nyakati tofauti, wadau kadhaa wamezungumza na kusema kuwa wameumizwa na kuguswa na tatizo la msanii huyo baada ya kutazama mahojiano kupitia Global TV Online. “Binafsi nimeguswa sana tatizo la Jini Kabula hivyo kwa chochote nitakachojaaliwa nitajitolea kwa ajili ya kusaidia kidogo, naamini na wengine wataguswa kama mimi, maana najua Watanzania tuna moyo wa upendo na mshikamano kwenye matatizo,” alisema mmoja wa wadau waliozungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wetu. Ndugu wa karibu wa Kabula wameliambia gazeti hili kuwa kwa yeyote aliyeguswa na tatizo hilo basi atume mchango wake kupitia namba 0712 56 53 69, ambapo jina litasomeka Daynes Jolwa ambaye ni dada wa Jini Kabula.

No comments: