Wednesday, September 13, 2017

DAKTARI BUGANDO AZUNGUMZIA HALI YA MC PILIPILI BAADA YA AJALI

Na Binagi Media Group Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Emmanuel Mathias (Mc Pilipili) amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu baada ya kupata ajali mbaya ya gari mkoani Shinyanga.

 Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Simon Haule amesema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa kumi alasiri katika Kijiji cha Mwanishoni, Kata ya Bubiki wilayani Kishapu katika barabara ya Mwanza-Shinyanga. Amesema ajali hiyo ilihusisha gari binafsi lenye nambari T.362 BAE Toyota Prado iliyokuwa na abiria watatu ikiendeshwa na dereva Said Hassan (28) mkazi wa Dar es salaam, ikitokea Mwanza kwenda Dar es salaam.

No comments: