MZIO (ALLERGY) TATIZO LINGINE LENYE UHUSIANO NA LISHE
kabla ya kuanza kuchambua mada ya leo, ni vyema tukajiuliza Mzio au kwa lugha ya Kiingereza Allergy ni kitu gani. Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, ‘Mzio ni hali ya kutoweza kula au kufanya kitu kwa kuchelea kudhurika’. Inakuwa mwiko kula au kufanya jambo fulani na unapovunja mwiko huo, madhara yake huonekana mara moja.
Inaaminika kuwa karibu kila mtu ana mzio na kitu fulani na hali hii inachukuliwa
Kuwa na mzio na kitu fulani, ni dalili kwamba hakuna uwiano mzuri mwilini na hali hiyo hunasababishwa na ukosefu wa virutubisho mwilini na kuishi staili ya maisha isiyofaa.
Ulaji mkubwa wa vyakula vilivyosafishwa (refined foods), ambavyo hupokonywa virutubisho vyake vya asili na vyakula vilivyotengenezwa na kuhifadhiwa kwenye makopo (proccssed foods), pamoja na kuishi maisha yenye msongo wa mawazo na mashaka, ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la mzio.
Vyakula vilivyotengenezwa na kuhifadhiwa kwenye makopo, sio tu hukosa virutubisho vyake vya asili, bali pia huwekewa kemikali nyingi za kuhifadhia vyakula hivyo, mara nyingi kemikali hizo (additives) huwa na madhara zinapojaa mwilini.
DALILI ZA MTU MWENYE MZIO
Dalili za mtu mwenye mzio zinazweza kutofautiana kati ya mtu na mtu, lakini kwa ujumla hali ya kuumwa kichwa mara kwa mara, kupata homa za mafua, kutapika mara kwa mara, kuharisha, kuvimba uso na macho ni miongoni mwa dalili za tatizo hili.
VIRUTUBISHO KAMA TIBA YA MZIO
Kuna aina fulani ya virutubisho ambavyo vimeonekana kuwa na uwezo wa kuzuia na kutibu tatizo la mzio. Mara nyingi ulaji wa Vitamin B5 au pantothenic acid huleta nafuu ya haraka kwa mwenye tatizo hili. Vile vile Vitamin E ina virutubisho vyenye nguvu kupambana na tatizo la mzio.
Kwa ulaji huo wa vitamin, unaweza kula vidonge maalum vyenye vitamin husika (food supplements) au kula lishe yenye kiasi kikubwa cha vitamin zinazohitajika na hupatikana kwa kula matunda na mboga za majani mchanganyiko na kwa kiasi kikubwa.
MAFUTA YA MBONO KAMA DAWA YA MZIO
Imegundulika kwamba mafuta ya mbono au nyonyo (castor oil), yana uwezo wa kutibu tatizo la mzio. Weka kiasi cha matone matano kwenye nusu kikombe chenye maji ya kunywa au juisi ya matunda ya aina yoyote, kunywa wakati wa asubuhi kabla hujala kitu chochote. Hutibu mzio wa kwenye utumbo, ngozi na mfumo wa kupumulia (pua na mdomo).
LIMAU KAMA TIBA YA MZIO
Limau nalo linaaminika kuwa na uwezo wa kutibu aina zote za mzio. Kamua kipande kimoja cha limau kwenye glasi, changanya na maji ya uvuguvugu kisha changanya na asali kidogo kupata ladha tamu kisha kunywa. Unaweza ukanywa mchanganyiko huo mara moja kila siku asubuhi kwa miezi kadhaa.
Limau siyo tu lina uwezo wa kuondoa sumu mwilini, bali pia lina uwezo wa kuzuia usipatwe na mzio. Hata hivyo wale watu wenye mzio na limau, machungwa na ndimu, wasitumie tiba hii, badala yake waangalie nyingine ambayo hawana matatizo nayo.
NDIZI KAMA TIBA YA MZIO
Ndizi mbivu moja au mbili kwa siku zina manufaa kwa wale wenye mzio kwa baadhi ya vyakula na ambao husumbuliwa mara kwa mara na matatizo ya kuwashwa na ngozi, kukosa choo, kusumbuliwa na pumu (athma). Hata hivyo wenye mzio na tunda hili nao wanashauriwa kuliacha.
JUISI YA MATUNDA KAMA
TIBA YA MZIO
Juisi ya matunda ina faida kubwa mwilini ikiwemo uwezo wake wa kuondoa tatizo la mzio. Tengeneza juisi ya matunda kwa kuchangaya karoti, kiazisukari (beetroot) na matango, tengeneza kiasi cha nusu lita na kunywa mara moja kwa siku hadi tatizo litakapotoweka.
FRESH JUISI KAMA TIBA YA MZIO
Njia bora kabisa ya kupambana na kuondoa tatizo la mzio mwilini, ni kuongeza kinga ya mwili ya kupambana na tishio lolote la mzio linaloweza kujitokeza. Kwa kuanza, fanya funga ya kunywa fresh juisi kwa muda wa siku nne mpaka tano. Baada ya hapo unaweza pia kuwa unaendelea na funga hiyo mara moja moja na kwa kufanya hivyo utaweza kutokomeza kabiza tatizo la mzio.
Baada ya funga ya juisi, anachotakiwa kufanya mtu mwenye tatizo la mzio, ni kuanza kujaribu kula mboga mboga aina moja baada ya nyingine. Akiona hakuna matokeo mabaya, aongeze tena aina nyingine ya chakula na kwa utaratibu huo anaweza kujikuta hana tatizo tena na chakula chochote.
Wakati wa kufanya zoezi hilo la kutokomeza mzio, vyakula vya kuepuka kabisa ni kahawa, chai, chokleti, soda, pombe, vitu vya sukari, vyakula vyenye kemikali na vyakula vya kutengeneza na kuhifadhi kwenye makopo. Kama una mzio na aina fulani ya chakula au tunda kama ilivyoorodheshwa hapo juu, tumia aina nyingine isiyo na mzio nayo hadi hapo tatizo litakapotoweka.
Mwisho, wenye matatizo ya mzio wanashauriwa kujiepusha na mawazo na kuishi maisha ya karaha ambayo huchangia mtu kupatwa na mzio. Aidha inashauriwa kufanya mazoezi ya kutuliza akili na kupumzika.
No comments:
Post a Comment