Monday, July 21, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Johari
Besta
Johari
Full Kujiachia: Utajiachia na nani?
Baada ya Ray C kuonekana kuwavutia wasomaji wengi wiki iliyopita kunako safu hii, Leo tunaendelea na ‘Full Kujiachia’, warembo watatu uwaonao pichani juu ni Besta, K-Lyini na Johari.

Unachotakiwa kufanya wewe msomaji ni kututumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na kutuambia kwamba, kama utapata nafasi ya kujiachia faragha na mmoja kati ya mastaa hawa utamchagua nani?

Anwani zetu ni zilezile, e-mail:wikienda@globalpublisherstz.com, simu 0713-403-202 na 0715-110 173. Kumbukeni kwamba, kila wiki tutakuwa tunachapisha maoni yenu bila kuwabania kwasababu tunaamini bila nyinyi safu hii haijasimama bado. Twenzetuni tusonge.

************************
Makamua:Hapa hazibanwi pua, ni sauti za ukweli
Pamoja na kuripotiwa na chombo kimoja cha habari siku chache zilizopita, kwamba amekula za uso katika matokeo ya mtihani wake wa kumaliza kidato cha sita, mchizi bado ameendelea kusimama vyema ndani ya game ya muziki wa kizazi kipya, Rebeka Bernard wa Ijumaa Wikienda alicheki naye.

Namzungumzia Mackpaul Sekimanga, ukimuita Makamua inakuwa poa ile mbaya. Akiwa na swahiba wake Joseph Calvin Mapunda Q-Jay kutoka kundi la Wakali Kwanza, wameandaa albamu ya pamoja waliyoipa jina la ‘Hazibanwi pua’, wakimaanisha kwamba sauti zao ni za ukweli, zinatoka moja kwa moja.

‘Ndani ya ‘Hazibanwi pua’ tumeweka nyimbo zetu zote zilizowahi kubamba na zinazoendelea kufanya vyema hewani. Inaweza ikawa albamu ya Bongo Flava yenye nyimbo nyingi zaidi kwasababu itakuwa na ngoma zaidi ya kumi na nane,” alisema Makamua.

Mshikaji alizitaja baadhi ya kazi zitakazokuwa ndani ya albamu hiyo kuwa ni Matatizo, Rudi, Ritha kwa nini umevunja gita, Maisha safari, Hazibanwi pua uliobeba jina la albamu na nyingine kibao.

*****************

King of HipHop: Nani kumfuata Kala?
Baada ya Kala Jeremiah kutupwa nje katika shindano la kumtafuta Ijumaa King Of Hip Hop wiki iliyopita, shindano linaendelea kusonga huku swali kubwa vichwani mwa mashabiki wengi likiwa ni nani atafuatia? Eunice Macha na Chausiku Omary wanashuka nayo.

Mpambano huo mkali na wenye upinzani wa nguvu kati ya wasanii waliochaguliwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho, umezidi kuwaweka roho juu hata mashabiki wanaofuatilia kwa karibu.

Mratibu wa Shindano hilo, Charles Mateso amewataka wasomaji waendelee kupiga kura zao ili kumchagua msanii ambaye wanaona anapaswa kutwaa taji la Ijumaa King of Hip Hop, ili mwisho wa siku apatikane mshindi wa kweli.

“Mshiriki ambaye atapata kura chache atalazimika kutoka kila wiki. Hivi sasa wamebaki wasanii tisa baada ya Kala kutoka ambao ni Fid Q, Chid Benz, Kalapina, Profesa Jay, Langa, Rado, Johmakini, Lord Eyes na Black Rhino. Wewe msomaji unaamini nani yuko juu kati ya hao? Endelea kupiga kura yako,” alisema Mateso.

Aidha mratibu huyo amesema kwamba wanachotakiwa kufanya wasomaji katika zoezi la upigaji kura ni kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa kuandika neno HP wanaacha nafasi, jina la msanii wanayehisi anapaswa kuwa Ijumaa King Of Hip Hop kisha wanatuma kwenda namba 15551.

*********************

No comments: