Monday, October 13, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ


Tupac:Hawa ndiyo mademu aliyowahi kujiachia nao
K utokana na maombi ya wasomaji wengi wa safu hii ambayo yanaendelea kumiminika kwa sana tangu tulipowaomba wafanye hivyo wiki iliyopita, leo tunawacheki mademu waliyowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na hayati Tupac Amaru Shakur.

Mashabiki wengi wa mwana Hip Hop huyo ambaye bado anaendelea kupata heshima mpaka leo kutokana na mchango aliyoutoa kunako game ya muziki huo enzi ya uhai wake, hawafahamu mchizi aliwahi kutoka faragha na warembo gani lakini ndani ya ‘Ebwana Dah!’ watapata kuwafahamu.

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘intaneti’, enzi za uhai wake Pac aliwahi kujiachia faragha na Arnelle Simpson, Faith Evans (ambaye ni mjane wa hayati Notorious B.I.G), Jada Pinkett Smith (ambaye sasa ni mke wa Will Smith), Jasmine Guy, Salli Richardson, marehemu Lisa Lopes a.k.a Left Eye, Janet Jackson (ambaye sasa ni mke wa Jermain Dupri), Rosie Perez, Madonna, Keisha Morris na Kidada Jones.

Tupac Shakur ambaye alifariki dunia katika Hospitali ya University Medical Center, Las Vegas, Marekani September 13, 1996 saa chache baada ya kupigwa risasi, akiwa na umri wa miaka 25. Bado tunaendelea kupokea maombi yenu wasomaji, ukitakana kufahamu staa gani wa nje, aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nani, tuandikie ujumbe mfupi kupitia namba 0715-110 173 au e-mail: wikienda@globalpublisherstz.com. Tupo kwa ajili yako msomaji.
*****************************************

Prof. Jay Kuwatoa nishai Lil Wayne, The game?
Kutoka Bongo tunayofuraha kuwafahamisha wapenda burudani na wapenzi wote wa sanaa ya Bongo Flava kwamba msanii Joseph Haule ‘Profesa Jay,’ ametajwa kuwania tuzo za MTV Afrika (Mtv Africa Music Awards with Zain) kama mwana Hip Hop bora akichuana na wakali wa Marekani, Lil Wayne na The game, Rebeka Bernard anatambaa nayo.

Akipiga stori na safu hii, mwakilishi wa Kampuni ya MTV Tanzania, Christine Mosha ‘Seven’ alitamka kwamba, michuano hiyo itafanyika Abuja, Nigeria Novemba 22, mwaka huu, huku mwakilishi wetu akitabiriwa kuwatoa nishai mastaa hao wa kiwanja.

“Mbali na Lil Wayne na The Game, Profesa Jay pia atachuana na wakali wengine kutoka Afrika, 9ice kutoka Nigeria na HHP wa Afrika Kusini katika tuzo hizo ambazo mdhamini wake mkuu ni Kampuni ya simu za mikononi ya Zain,” alisema Seven.
Aidha, Seven alisema kwamba, wakati washindi wa tuzo hizo wakitangazwa huko Velodrome, Abuja, Nigeria Novemba 22, 2008 kupitia Mtv Base, (DStv Channel 322), hapa Bongo mpambano huo utakwenda hewani kupitia Kituo cha Televisheni cha TBC1.
Fiesta ‘08: A-Town kupagawa kesho
Baada ya kusubiri kwa hamu kubwa, wapenda burudani wa A-Town (Arusha) kesho watajilamba na Fiesta 2008 ambayo itadondosha bonge la shoo litawapagawisha ndani ya Ukumbi wa Matongee Carnival Park, uliyopo Njiro mkoani humo.
Mashabiki hao wataua ndege kibao kwa jiwe moja, yaani shoo hiyo itadondokea Oktoba 14, ambayo itakuwa ni kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. JK Nyerere.

Wasanii kibao watasababisha siku hiyo kwa shoo nyingi za laivu, nawazungumzia Ray C, Chid Benz, Marlaw, Mwasiti, Nako 2 Nako, Johmakini, Dully Sykes, Prof Jay, A.Y, Q Jay, TMK Wanaume Halisi, Nyota Ndogo kutoka Kenya na wengine wa kutosha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa waratibu wa tukio hilo, Godfrey Kusaga, kiingilio kunako shoo hiyo ni shilingi elfu tano na baada ya hapo msafara utaelekea Mkoani Mbeya kwa shughuli moja ya nguvu ambayo itapigwa ndani ya Ukumbi wa Dhandhu.
*************************
Bonanza la wafungwa kufanyika kesho
Hayawi, hayawi sasa yamekuwa! Lile Bonanza la Wafungwa lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers kupitia gazeti lake la michezo la Championi, linatarajiwa kufanyika kesho katika Viwanja vya ndani vya Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam, Chausiku Omary anashuka nayo.

Mratibu wa Bonanza hilo ambaye pia ni Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Isaac Kijoti jana Ofisini kwake Sinza, Bamaga jijini Dar es Salaam alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwa ni pamoja na kupata kibali.

“Ni kweli kesho Oktoba 14 siku ambayo ni ya kukumbuka kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere ndiyo mambo yote yatafanyika, kwani kwa taarifa niliyoipata kutoka kwa Naibu Kamishina wa Magereza nchini, Salum Chambuso ni kwamba wafungwa nao wamejiandaa vema kutoa burudani na michezo mbalimbali.

“Taarifa kamili tutaitoa Jumatatu (leo) katika mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika Makao Mkuu ya Magereza Posta jijini Dar es Salaam saa sita mchana na kuhudhuriwa na Kamishina Mkuu wa Magereza nchini, Augustino N. Nanyaro,” Kijoti alifafanua.

Mbali na kuwashukuru wadau mbalimbali waliochangia na kufanikisha zoezi hilo, pia alisema milango bado ipo wazi kwa wale wote watakaopenda kuchangia.

“Tunaomba wale wote watakaopenda kujitolea vitu kama sabuni, dawa za mswaki, miswaki, mafuta ya kujipaka au vifaa vya michezo kujitokeza kwani bado tunavipokea kwa ajili ya kuwakabidhi kesho katika bonanza hilo,” alifafanua mratibu huyo.

Katika tamasha hilo, Nguza Vicking pamoja na wanawe watapanda jukwaani kushusha burudani ya kukata na shoka huku wafungwa wengine wakionesha umahiri wao wa kusakata dansi pamoja na miamba miwili Simba na Yanga gerezani hapo itatoana jasho dimbani. Yeyote anayependa kuchangia shughuli hiyo apige simu kwa Kijoti, kwa namba 0787-057 057.

1 comment:

Anonymous said...

Bwana Mrisho habari ya kazi. Habari zingine ukiwa unaziandika jaribu kwanza kuzifanyia uchunguzi wa kutosha. Jada Pinkett-Smith hajawahi kutoka na Tupac. Kwa wao kuigiza katika sinema pamoja hakufanyi watu kuwa wapenzi hata kama walicheza scene ya mapenzi. Kwa taarifa yako Tupac hajwahi kutoka na Jada. Nimekumegea kipande kidogo tu kutoka kwenye biography ya Jada. siku njema.


In the documentary Tupac: Resurrection, Tupac Shakur says, "Jada is my heart. She will be my friend for my whole life." Also in this documentary, Pinkett Smith calls Shakur "one of my best friends. He was like a brother. It was beyond friendship for us. The type of relationship we had, you only get that once in a lifetime." The two remained close friends until 2Pac Shakur's death in 1996. After graduating from the Baltimore School for the Arts, Pinkett Smith then spent a year at the North Carolina School of the Arts before dropping out to pursue her career in acting. Pinkett Smith is an honorary member of Alpha Kappa Alpha Sorority Inc.