Friday, September 26, 2008

Ijumaa KIng of Hip Hop: Top 05



Kutoka ndani ya shindano la kumtafuta Ijumaa King Of Hip Hop, tunayofuraha kubwa ya kuwataja rasmi washiriki waliyofanikiwa kuingia katika tano bora, hatua ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa.

Kwa mujibu wa mratibu wa mpambano huo, Charles Mateso washiriki waliyopasua mpaka ‘Top 5’ ni Johmakini, Chid Benz, Fid Q, Kalapina na Profesa Jay ambao kwa pamoja wameingia katika hatua ya fainali itakayomtoa mshindi mmoja, yaani Ijumaa King Of Hip Hop.

“Tunawaomba wasomaji na wapenzi wa muziki wa Hip Hop waendelee kutuma kura zao wakituambia nani anastahili kuwa bingwa. Wanaandika neno HP (wanaacha nafasi) wanaandika jina la mshiriki ambaye wanadhani anastahili kuwa mshindi, kisha watume kwenda namba 15551,” alisema Mateso.
***************

Wednesday, September 24, 2008

another day, another surprise!


Popular SuperSport presenter Thomas Mlambo is comfortable in the presence of sports stars, having interviewed many of them during a television career that has spanned more than 10 years. From Brazilian legend Pele to African superstars, Mlambo has never been intimidated by the big names of football.

The SuperSport studio is like a second home to him and his relaxed demeanour in front of the camera has earned him scores of admirers across the African continent.

But his biggest challenge lies just ahead. On Saturday September 27, Mlambo will make an appearance in the Big Brother Africa house from 11:30 to 14:30 CAT, during which the theme will be SA 2010 and the task for the housemates will be World Cup related.

“It will be interesting to see if the winner of the ‘Big Brother World Cup’ challenge goes on to rule the roost at the end of the competition, especially with football being so huge on the continent,” said Mlambo.

“I don’t feel I’ll be intimidated going into the house, it is more of a ‘fear factor’ feeling for me, but I am really looking forward to the experience!”

Tune in to Big Brother Africa on DStv channel 198 to see how Mlambo handles the personalities that have become part of our daily lives in recent weeks.

AINA ZA FUNGA

Wiki hii tunaendelea tena na makala yetu kuhusu funga kama tiba na kinga ya maradhi mbalimbali mwilini. Wiki iliyopita tuliona jinsi funga inavyoweza kuondoa sumu mwilini na faida nyingine nyingi kama zilivyothibitika kisayansi. Wiki hii tutaangalia aina za funga zilizopo pamoja na mambo mengine, endelea…

AINA ZA FUNGA
Kuna aina kadhaa za funga ambazo mtu anaweza kuzitumia kwa lengo fulani. Funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni funga ya ibada, ambapo mfungaji anapata thawabu kwa Muumba wake lakini pia anapata faida za kiafya za ujumla zinazotokana na funga.

Aina hii ya funga inajulikana pia kama DRY FAST, kwa maana mtu hatakiwi kula wala kunywa kitu chochote kuanzia alfajiri hadi magaharibi jua linapozama, kwa muda wa siku 30 au 29. Mfungaji wa funga aina hii, licha ya kuwa ni ibada, anapata pia faida zote za kiafya tulizozieleza hapo juu.

Bila shaka mpenzi msomaji, kama nawe uko kwenye funga ya mwezi huu, unaweza kuwa shahidi wa faida zinazopatikana kiafya kutokana na kufunga, inawezekana hivi sasa husumbuliwi sana na presha, kisukari au kuumwa na kichwa kama inavyokuwa siku za kawaida.

Aina nyingine ya funga ni ile funga ya kawaida ambayo pia inajulikana kama RUGULAR FAST. Katika funga hii, ambayo hufungwa ili kutimiza malengo ya kiafya tu, mtu hali chakula bali hunywa maji mengi ili kuyeyusha sumu mwilini na kuitoa kupitia kwenye ngozi na figo.

Funga nyingine ya malengo ya kiafya ni ile ya kufunga kula vyakula vyote ispokuwa juisi za matunda tu, funga ya aina hii, ambayo pia hujulikana kama FRUIT JUICE FASTING, mtu hunywa juisi za matunda ya aina mbalimbali kwa siku kadhaa na ni njia ya uhakika ya kuondoa sumu zote mwilini na kuuacha mwili wako ukiwa safi na wenye ngozi nyororo.

Katika funga hii, inashauriwa kwa mfungaji kutokunywa juisi bila kuichanganya kidogo na maji, kwani bila kufanya hivyo inaweza kuvuruga mchakato wa usagaji chakula mwilini. Changanya nusu ya juisi yako na nusu ya maji baridi, lakini kamwe usichanganye na barafu au maji yaliyoganda.


DALILI ZINAZOJITOKEZA WAKATI WA FUNGA
Wakati wa funga kuna dalili kadhaa hujitokeza kwa mfungaji. Dalili hizo ni pamoja na tumbo kuwa na gesi na kuunguruma, kuongezeka na kisha kushuka kwa joto la mwili, mdomo kuweka utandu mweupe, kutapika na jasho kutoa harufu kali.

Dalili zote zilizotajwa hapo juu siyo mbaya bali zinaashiria habari njema kuwa mwili uko katika mchakato wa kujisafisha na kuondoa sumu iliyokuwa imeganda na kujikita kwenye mfumo wa mwili kwa muda mrefu.

FUNGA INADHOOFISHA MWILI?
Si kweli kwamba funga hudhoofisha mwili. Imegundulika kwamba kinachomkondesha mtu wakati wa funga ni woga na mara nyingi vitu tunavyoviogopa katika maisha yetu huwa vinatuaathiri. Baadhi ya watu wanaogopa kufunga kwa dhana kwamba mtu huwezi kushinda bila kula, unaweza kufa - kitu ambacho si kweli na ndiyo kinachowakondesha baadhi ya watu.


JINSI YA KUFUNGUA

Faida kubwa inayopatikana kutokana na kufunga inaweza kupotea na kusababisha madhara kama kanuni za kufungua hazitazingatiwa. Kwa kawaida wakati wa kufungua, kwa mfano magaharibi kwa waislamu, watu hukimbilia kula vyakula vya kila aina na kwa kiasi kikubwa.


Kwa hakika, faida ya funga inapatikana kwa aina ya chakula utakachokula baada ya kufungua na jinsi gani utakavyoweza kujizuia kula vyakula visivyosahihi. Wakati wa kufungua mtu anapaswa kuanza kwa kula vyakula vya asili kama vile juisi, matunda, maji, ambavyo havina kemikali za zumu na baada ya hapo kula mlo ulio sahihi na kwa kiasi cha kawaida.

Ni makosa makubwa kufungua kwa kuingiza tena sumu mwilini, kama vile kufungua kwa kuvuta sigara, kula mishikaki au vyakula vingine vilivyopikwa na mafuta mengi. Aidha, mtu anayefungua anatakiwa, si tu kula vyakula vya asili, bali pia kula kwa kiasi na siyo kula kupita kiasi kwa lengo la kufidia mlo wa mchana kutwa!

Mwisho kabisa, inashauriwa mfungaji kuendelea kuzingatia kanuni za ulaji sahihi, funga itakuwa haina faida yoyote kiafya iwapo wakati wa kufungua unakula kila aina ya chakula unachokiona mbele yako tena kwa kiwango kikubwa, itakuwa sawa na kujaza maji kwenye gunia.

Nawatakia funga njema waislamu wote duniani na Mungu awabariki!

Tuesday, September 23, 2008

LATOYA HUYOOO!!!


Hatimaye Latoya ametua Bongo na kesho atakuwa na press kueleza nini kilitokea mpaka akawa wa kwanza kutolewa badala ya wa mwisho kama ilivyosiku zote kwa Tanzania. Pichani akiongea na Seven ambaye alikuwa mwakilishi wa Mnete nchini kwa utangazaji.

Monday, September 22, 2008

SHINDA BENZ KWA KUSOMA!

WIKIENDA SHOWBIZ!

Mwana FA: Sifikirii kujibizana na Inspector Haroun

Msanii Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ ambaye wiki iliyopita alizushiwa kifo, ameamua kuongea kidogo kuhusiana na ngoma mpya ya Haruna Kahena ‘Inspector Haroun’, ‘Bado upo upo’ ambayo ni kama jibu la wimbo wake, ‘Bado nipo nipo’ kwa kusema kwamba hapendi kujibizana na mchizi huyo, isipokuwa amekerwa na baadhi ya maneno aliyotumia kunako songi lake, ambayo ameyafananisha na matusi.

Akipiga stori na safu hii kwa njia ya simu, Mwana FA alisema kwamba hafikirii kwenda katika vyombo vya habari kwa ajili ya kujibizana na ‘Inspector’, kwasababu alichoimba ni mawazo yake na wala hakuongelea habari za ndoa, wala hakusema watu waachachane kama alivyoimba msanii huyo kutoka TMK.

“Mimi sijazungumzia ndoa, wala kuwataka wanandoa waachane, isipokuwa katika wimbo wangu kuna sehemu nimesema kwamba, watu wanalalamika, wanapoumizwa na ndoa zao, wengine wanaficha, wanakufa na maumivu yao, siwezi kumshangaa sana inawezekana anataka kutokea mgongoni kwangu, lakini kilichonikera ni jinsi alivyonitukana katika wimbo wake,” alisema Mwana FA.

Aidha, Mwana FA alisema kwamba, siku chache zijazo anatarajia kukwea pipa na kwenda kupiga shoo Uingereza na Scotland na mara atakapodondoka Bongo ataachia ngoma nyingine yenye jina la ‘Naongea na Wewe’ ambayo video yake itafanyika nchini Kenya kupitia Kampuni ya Ogopa. “Mpaka mwishoni mwa Oktoba, video na wimbo huo vitakuwa hewani”.
Baadhi ya mashabiki wa muziki wa Bongo Flava waliopiga stori na safu hii, wameikandya tabia ya Inspector kupenda kujibu nyimbo za wasanii wengine kuwa siyo ‘freshi’ na kwamba anaonesha ni jinsi gani alivyoishiwa katika game, kitu ambacho pia kinaweza kumshusha kisanii.
***************************************************
STREET VERSION:
Wiki hii ‘Street Version’ haitakuwa na staa wa Kibongo, badala yake ilizama kunako mtandao wa ‘intaneti’ na kufanikiwa kuzibamba picha za mastaa wa muziki wa R&B, Chriss Brown na Rihana wakikatiza katika mtaa mmoja uliyopo Marekani, wakifanya ‘shopingi’.
Hivi sasa mastaa hao wameamua kujiachia na kuweka mapenzi yao hadharani tofauti na siku za nyuma ambapo walikuwa wanaficha. Hebu cheki picha hapo chini, ni kama vile walikuwa wanaongea...



compiled by: MC George

Sunday, September 21, 2008

Latoya OUT! Awaaibisha Watanzania!


Mshiriki wa Tanzania kwenye Shindano la Big Brother III, Latoya Lyakurwa amedaiwa kuponzwa na vitu vitatu ndani ya mchuano huo unaoendelea nchini Afrika Kusini.

Kitendo chake cha ‘kukandamiza malavidavi’ na Ricco wa Angola ni pointi ya kwanza ambayo ilimuondolea sifa ya kuendelea kubaki ndani ya mjengo.

Pointi ya pili ni pale aliponaswa na kamera akila denda na Moris wa Uganda, wakati huo huo mara kadhaa akawa anachojoa mbele ya wenzake, tabia ambayo haiendani na maadili ya Mtanzania na Muafrika kwa ujumla.

Kufuatia hali hiyo, Latoya atatakiwa kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kuchafua ‘hali ya hewa’ ndani BBA ambayo ilisafishwa vizuri na Mwisho Mwampamba mwaka 2003 na Richard Bezuidenhout mwaka jana.

Pamoja na hivyo Jumamosi iliyopita, Latoya alionesha uzalendo wa kutosha kwa kuzifagilia baadhi ya kazi za wasanii, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Joseph Haule ‘Prof. Jizze’ ambazo zilionesha kumpagawisha kwa sana.

chumba maalum walimowekwa na Tawana wa Botswana wakati wakisubiri mmoja wao kutoka, akiweka CD zenye nyimbo za wasanii hao na kucheza kwa hisia.

Mbongo huyo ambaye kwa upande mwingine alionekana kama amekumbuka nyumbani alianza kupagawa na ngoma za Mwana FA, ikiwemo inayotamba hivi sasa, ‘Bado Nipo nipo’, kisha akabadilisha na kuweka CD yenye nyimbo za Profesa Jay, kitu ambacho kilimfanya apandishe mzuka zaidi wa kucheza na kuimba, hasa aliposikia kazi kama ‘Hapo Vipi’, ‘Ndivyo sivyo’ na ‘Nang’atuka’.

Pamoja na mabaya yote aliyoyafanya mjengoni humo, safu hii inampa ‘big up’ za kutosha Latoya kwa kuonesha uzalendo huo wa kuzifagilia na kuzipa promo kazi za Wabongo wenzie. Wakati huo huo, mshiriki kutoka Kenya, Sheila anaendelea kupeta kimapenzi na Takondwa ‘TK’, kitendo kinachowafanya washiriki wengine wakae wakinong’ona juu yao.

Latoya OUT! Awaaibisha Watanzania, Prof. Jay, Mwana FA wampagawisha

Mshiriki wa Tanzania kwenye Shindano la Big Brother III, Latoya Lyakurwa amedaiwa kuponzwa na vitu vitatu ndani ya mchuano huo unaoendelea nchini Afrika Kusini.

Kitendo chake cha ‘kukandamiza malavidavi’ na Ricco wa Angola ni pointi ya kwanza ambayo ilimuondolea sifa ya kuendelea kubaki ndani ya mjengo.

Pointi ya pili ni pale aliponaswa na kamera akila denda na Moris wa Uganda, wakati huo huo mara kadhaa akawa anachojoa mbele ya wenzake, tabia ambayo haiendani na maadili ya Mtanzania na Muafrika kwa ujumla.
Kufuatia hali hiyo, Latoya atatakiwa kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kuchafua ‘hali ya hewa’ ndani BBA ambayo ilisafishwa vizuri na Mwisho Mwampamba mwaka 2003 na Richard Bezuidenhout mwaka jana.
Pamoja na hivyo Jumamosi iliyopita, Latoya alionesha uzalendo wa kutosha kwa kuzifagilia baadhi ya kazi za wasanii, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Joseph Haule ‘Prof. Jizze’ ambazo zilionesha kumpagawisha kwa sana.

chumba maalum walimowekwa na Tawana wa Botswana wakati wakisubiri mmoja wao kutoka, akiweka CD zenye nyimbo za wasanii hao na kucheza kwa hisia.
Mbongo huyo ambaye kwa upande mwingine alionekana kama amekumbuka nyumbani alianza kupagawa na ngoma za Mwana FA, ikiwemo inayotamba hivi sasa, ‘Bado Nipo nipo’, kisha akabadilisha na kuweka CD yenye nyimbo za Profesa Jay, kitu ambacho kilimfanya apandishe mzuka zaidi wa kucheza na kuimba, hasa aliposikia kazi kama ‘Hapo Vipi’, ‘Ndivyo sivyo’ na ‘Nang’atuka’.
Pamoja na mabaya yote aliyoyafanya mjengoni humo, safu hii inampa ‘big up’ za kutosha Latoya kwa kuonesha uzalendo huo wa kuzifagilia na kuzipa promo kazi za Wabongo wenzie. Wakati huo huo, mshiriki kutoka Kenya, Sheila anaendelea kupeta kimapenzi na Takondwa ‘TK’, kitendo kinachowafanya washiriki wengine wakae wakinong’ona juu yao.