Friday, August 14, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

washindani hawa hapa
Yusuf Mlela, Lawrence Malima ‘Marlaw’, Tundaman, Hemed, Chid Benz, Ray, Kanumba, Mwisho Mwampamba, Black Rhino na AY ni majina 10 ambayo yamepata kura nyingi zaidi ili kuendelea kwenye shindano.

Hata hivyo, lengo ni kupata majina 12 ili kuchapa mwendo kuelekea kumpata mshindi. Majina yafuatayo, yamepata kura zinazolingana kwahiyo kati yao, unatakiwa kutuma sms ukitaja jina la mmoja wao ili wawili waungane na wenzao hapo juu.

Spark, Makamua, Jerry Tegete na Danny Mrwanda kati yao tuma machaguo mawili, watakaoongoza wataungana na wenzao 10. Dondosha kura kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) kupitia simu namba 0787-110 173, e-mail:mcgeorge2008@gmail.com, ili shindano lianze kuchapa mwendo.
*** *********************************************

Steve
Bwa mdogo mwenye vocal inayokamata, Steven William ‘Steve’ ndiye artist anayeng’ara zaidi hivi sasa Bongo na kuzidi kuiweka R&B juu ya mstari.

Traki inayokwenda kwa jina la Sogea Karibu ambayo Steve ameifanya pamoja na Dataz inabamba namba moja katika singo zote za R&B ambazo zinapasua anga kwa sasa, hiyo ni kwa mujibu wa tathmini ya ShowBiz.

Janki huyo ambaye anapatikana kwenye lebo ya Zizzou Entertainment, ameanza kukamata hapa juzi kati hasa baada ya kufanya wonderful chorus katika ngoma ya Tabasamu aliyopewa shavu na Heri Samir ‘Blu’ lakini janki amekwishafanya mengi katika industry.

Hivi sasa amekwishakamilisha mawe nane ambayo anatarajiwa kuyajaza katika albamu yake ya kwanza.

“Muda si mrefu nitaachia wimbo wangu mwingine unaoitwa Baby Girl ambao nimefanya na Ngwair, hii ni baada ya kuona Sogea Karibu umekubalika,” alisema Steve.
Do u need more from Steve? Stay tuned.
****************************************

Tears On Valentine day: wasanii waingia mzigoni kupiga picha
Ile muvi ya kijanja, itakayosheheni wasanii wa ukweli, yaani vipaji asilia imeanza kurekodiwa katika allocation za Jiji la Dar, ebwana eeh!

Showbiz imepewa mnuso huu na Mkurugenzi wa Filamu wa Tollywood Movies, Hamie Rajab kwamba mambo yanapamba moto na kuongeza kuwa staili ya kurekodi uhondo mzima ni ya aina yake.

Hamie alisema kuwa kilichomvutia zaidi ni kuona kwamba zoezi ambalo Tollywood ilifanya la kusaka wasanii wenye vipaji kwa ajili ya filamu hiyo limekuwa ni lenye faida kubwa.

“Tumepata wasanii ambao wanaonesha uwezo mkubwa, yaani hawamsumbui mwongozaji wakati wa kurekodi wakiambiwa kitendo wananasa papohapo, hayo ndiyo matunda ya vipaji,” alisema Hamie.
*******************************************
COMPILED BY MC GEORGE

No comments: