Monday, March 8, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Karrine Steffans: Ni full ngono, usagaji na kuwabemenda serengeti boys!
Ebwana Dah! Actress Karrine Steffans anatoa kishindo cha nguvu, idadi ya watu aliokwea nao on bed kwa ajili ya ngono ni mshtuko wa aina yake.

Muhimu ni kwamba Karrine ameonesha uwezo mkubwa siyo tu wa kuvunja amri ya sita, bali pia usagaji na kwenda the same style na watoto wadogo kwa umri a.k.a kuwabemenda.

Andre 3000 anatajwa wa kwanza, Big Boi ndani, marehemu Big Pun naye alisuuza kisela, akaja Black Thought, hard vocalist, Busta Rhymes alipumzika, Canibus alipewa hifadhi, Chris Rock pia alijikunja nae.

Karrine aliona wanaume is not an issue akaamua kusagana na Da Brat, baadaye akageukia kwa Fred Durst, hakuona noma kumsaulia Havoc, mchizi Ja Rule akaonja joto la huba, Baba Beyonce, Jay-Z naye alipewa, Juelz Santana akamega kimtindo, Larenz Tate pia alifanya kweli.

Method Man, Mos Def, Mr. Marcus, Mystikal, Nas, P Diddy, Q-Tip, Redman, Russell Simmons, Snoop Dogg, Talib Kweli, Timbaland, Usher Raymond, Xzibit, Kool g. Rap, Common, Vin Diesel, Bobby Brown, Young Buck, Shaquille O`Neal, Bill Maher, Darius McCrary wote hao walipita kwa kupishana.

Kama hiyo haitoshi, Karrine akaamua kuwabemenda Serengeti boys, Ray-J na Bow Wow. Alizaliwa St. Thomas, U.S. Virgin Islands, Marekani, Agosti 24, 1978, ni muumini wa madhehebu ya Born-Again Christian.
***************************

Dudu
Dogo Hamidu

Ali Kiba
Bongo Flava :Appreciation ni msamiati mgumu kwao!
Msaada ni sehemu ya maisha, usiposaidiwa basi wewe utasaidia. Kusaidiwa is not a scandal ni hali ambayo hutokea. Hata tajiri nambari moja duniani Warren Buffet anasaidiwa, ingawa yeye ndiye the best philanthropist duniani, itakuwa wewe mwana Bongo Flava?

Utafiti uliyofanywa na Abby Cool & MC George over the weekend umegundua kwamba wasanii wengi wa muziki wa Bongo Flava hawataki kujulikana kama wanasaidiwa. Zay B aliwahi kumkataa Inspector Haroun kwamba hajampa ‘tafu’ kwa lolote, ingawa ipo wazi kuwa bila vocal ya kikatuni ya Babu, Gado isingesimama.

Talk of the nation at large ni tamko la Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ kwamba akiwaona undergrounds huwa anapata kichefu chefu kwa sababu huko nyuma alijitahidi kwa uwezo wake wote kusaidia vijana wenye vipaji but walipoota meno wakamng’ata yeye.

Aliwataja wengi ambao aliwapa msaada, Nyandu Tozz a.k.a Dogo Hamidu, Afande Sele, Pig Black na wengine wa kumwagililu! Nini hiki? Shukurani ni msamiati mkubwa.

Kwa wale wanaofahamu where Bongo Flava come from, wanaelewa Nyandu au Dogo Hamidu ni mwana aliyekulia kwenye mikono ya The Dudu lakini baada ya janki kutoka Sauzi imekuwa tabu kweli kweli.

Tatizo si Nyandu, bali ni utamaduni wa wasanii wetu, hawaelewi kwamba kusaidiwa ni sehemu ya maisha ya kila binadamu, Eminem alisaidiwa na Dr. Dre halafu na yeye ndiyo akaja kumtoa 50 Cent, kila mmoja ana-appreciate tafu aliyopewa.

Father P anaandika nyimbo lakini madogo wakiimba hawataki ijulikane kama wameandikiwa. Hili ni tatizo la uelewa mdogo, wanashindwa kujua kwamba hata Michael Jackson ambaye ni mfalme wa mauzo ya muziki, naye aliwahi kuandikiwa baadhi ya ngoma zake.

Haishangazi kusikia leo Fid Q anakataa kwamba hajawahi kusaidiwa na Sir Nature au Hardmad, lakini ukweli unajulikana kuwa safari ya Ngosha a.k.a The Don Himself kutoka Zoo hadi staa anayekubalika, amepata msaada mkubwa.

Huko kiwanja, mastaa hawaoni aibu kusema kuwa wamesaidiwa, 50 huwa anamtaja Eminem au Bow Wow kwa Snoop Dog na JD. Mase hajawahi kubanduka ngozi kwa kuwataja P Diddy na B.I.G kuwa ndiyo waliomtoa.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, msanii mmoja wa Temeke anayeitwa Maliki aliandikiwa wimbo na ‘The Bid Base’ Solo Thang a.k.a Ulamaa, lakini mchizi alipojipa shavu kuwa yeye ndiye mwandishi, zikataka kuruka ngumi. Tatizo kubwa!

Ni vema kubadilika sasa, wasanii watoe shukurani kwa misaada wanayopewa. Kukataa kwamba hujasaidiwa maana yake unaziba mianya ya wale wa chini kupigwa tafu, si unajua mtu akigongwa na nyoka, akiguswa na jani anashtuka? The Dudu anasema ni kichefu chefu.

Last Friday katika kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa hewani na Channel 5, The Dudu na Nyandu walikutanishwa na wakasuluhishwa na mtangazaji Jimmy Kabwe, lakini kilichotokea ni unafiki.

The Dudu alisema anamchukulia Nyandu kama mwanaye, kamlea wakati Nyandu alidai yeye hana matatizo na Dudu ila magazeti. Nini? Ilikuwa ni unafiki, alipaswa kukiri matamshi yake kwanza badala ya kuelekeza lawama kwenye magazeti. Tuelewane, kusaidiwa siyo skendo, ni sehemu ya maisha.
******************************

Njoshi

‘Uprezidaa wa akina Nyoshi feki’
Mkongwe kwenye eneo la kucharaza gita, Elyston Angay ambaye ni kiongozi wa Bendi ya Mashujaa a.k.a Vibration Sound amesema kuwa mtindo wa akina Nyoshi El-Saadat, Christian Bella kujiita maprezidaa ‘full utani’ kwa sababu Tanzania Rais ni JK only.

Katika special interview na safu hii, iliyochukua nafasi Posta, Dar last week, Angay alisema kuwa guys wanaopenda kujiita ni maprezidaa kwa sababu wameaminiwa na bendi zao kuziongoza, lengo lao si lingine bali ni kujipa ujiko usio na maana yoyote.

“Rais ni Kikwete tu hao wengine wababaishaji na akipita nchi inajua hapa rais kapita, sasa wewe hata hapo mtaani kwako ukipita watoto ndiyo wanajua umepita, walevi wanakutukana hovyo, huo ni urais gani? Tuacheni dharau kwenye vyeo vya watu,” alisema.
compiled by mc george/Ijumaa Wikienda

1 comment:

Anonymous said...

Abdallah mrisho sijapenda topic zako za kuwatoa wanawake stars kuwa wamelala na wanaume wangapi kila siku. What is your motive behind ni kwamba msiwaone wanawake ni wachafu au? Mbona sijawahi kuona ukiweka wanaume wamelala na wanawake wangapi au hata wale wanasadikika kuwa ni mashoga na ni watu mashuhuri wakubwa tu kwenye tasnia ya muziki. Unatudhalilisha aidha uache au ubalance uweke na wanaume wachafu