Friday, May 28, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

ETRA BONGO: Kujinadi Msasani Club leo
Wanamuziki wanaounda Bendi ya Extra Bongo a.k.a Next Level ‘Wazee wa Mjini Mipango’ chini ya uongozi wake ‘Prezidaa’ Ally Choki leo ‘Mzee wa Farasi’ katikati ya wiki hii walidondoka ndani ya mjengo wa magazeti pendwa, Global Publishers na kuyoa shukrani zao huku wakiitaja siku ya leo (Ijumaa) kuwa ni maalum kwao kwani wako tayari kujitambulisha rasmi.

Wakiwa ndani ya Global Publishers ambao ni wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Amani, Championi, Ijumaa wikienda, Risasi na hili (Ijumaa), Ally Choki alisema kwamba wana kila sababu ya kuishukuru kampuni hiyo kwa jinsi inavyojitoa kuwasapoti wasanii mbalimbali ikiwemo Bendi ya Extra Bongo.

“Naomba muendelee kuwa pamoja nasi ili kutuinua zaidi na kuutangaza muziki wetu mbali. Pia nachukua fulsa hii kuwaambia mashabiki wetu kwamba Mei 28, mwaka huu (leo Ijumaa) ni siku yetu ya kuzaliwa upya, tutafanya utambulisho wa bendi pamoja na albamu yetu mpya ‘Mjini Mipango’ pale ndani ya Ukumbi wa Msasani Club, Dar es Salaam,” alisema Choki.

Katika uzinduzi huo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa burudani, Extra Bongo watasindikizwa na vichwa kibao akiwemo akiwemo mchizi kutoka Congo DRC, Adof Domingezi akiwa na bendi yake, Wenge Tonyatonya. Wengine kutoka Bongo ni pamoja na Profesa Jay, Matonya, Hussen Machozi na wasanii wapya kutoka Kiumbe record.

Choki alisema wameamua kuitambulisha rasmi bendi hiyo ili kuwafanya mashabiki wafahamu ratiba na jinsi mchakato utakavyokuwa ili kukata kiu ya burudani kwa wapenzi wa muziki huo. Uzinduzi huo umedhamini wa kampuni ya Global Publishers kupitia shindano la Shinda Toyota Vitz Awamu ya pili itakayonadiwa vema leo ukumbini hapop.
*******************************************
A.Y kupiga kolabo na Sean Kingston
Kama ulikuwa haujafahamu ,kuna bonge la ishu limedondoka pande hizi likitengeneza kichwa cha habari kisemacho kwamba, A.Y kupiga kolabo na Sean Kingston, ikiwa na maana kwamba siku kadhaa zijazo mchizi atakwea pipa na kwenda kupeperusha bendera ya Bongo katika nchi ya Obama kwa kufanya kazi na staa huyo.
Picha lilianzia ndani ya kituo cha Redio Cloud FM pale Sean Kingston alipokuwa anafanyiwa ‘intavyuu’ kupitia kipindi cha XXL muda mchache baada ya kuwasili Bongo kwaajili ya shughuli nzima ya utoaji tuzo za Kili iliyofanyika hivi kariubuni.

Ndani ya ‘intavyuu’ hiyo ambayo ilirekodiwa kwenye video ya Frank Mtao wa 2Eyez Production, Sean Kingston alisema kwamba msanii wa Bongo anayemkubali zaidi ni A.Y na kwamba alitamani kuangusha naye kolabo, kitu ambacho kiliwafanya wasaidizi wake wawasiliane na Mzee wa Commercio ambaye alipata ‘chansi’ ya kukutana na staa huyo kisha kubadilishana mawazo.

“Nilipokutana na jamaa kweli alisema anavutiwa na kazi zangu, akaniomba tukapige kolabo, ni mtu ambaye hana mapozi na ilikuwa nipige naye ngoma moja hapa Bongo lakini bahati mbaya prodyuza wangu, Hermy Bakawa amesafiri. Kwa kifupi amenipa moyo sana, nikienda huko natarajia kufanya maajabu,” alisema A.Y ambaye hivi karibuni ametajwa kuwania tuzo tano zitakazotolewa nchini Ghana Juni mosi mwaka huu. Unaweza kumpigia kura kupitia www.awards.museke.com.

No comments: