Monday, May 31, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Mayweather na Keyshia Kole mambo safi
Sugu: Antivirus ya kirusi cha Bongo fleva ipo jikoni
Kaka Mkubwa wa Bongo Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ amewakusanya wana kibao na kuanzisha very active project inayokwenda kwa jina la Antivirus.

Project hiyo inahusu mapinduzi, inanyoosha ukweli kwa vipimo vyake, inawagonga fatuma wezi wote waliohusika kuihujumu Bongo Fleva na inatangaza vita kwa yeyote mwenye shida ya ubaya dhidi ya wanamuziki wataka haki. Mr. II a.k.a Sugu alitinga kwenye mjengo wa Global Publishers (GPL) akiwa ameongozana na super characters wa Antivirus, Fredy Maliki ‘Mgosi Mkoloni’, Danny Msimamo na Dotto Maujanja kutoka crew ya mapacha.

Antivirus ni project ya mashambulizi mwanzo mwisho, itafanya kazi kwa mtindo wa mixtapes, yaani kurekodi nyimbo kwenye instruments maarufu za kiwanja, halafu ngoma zinawekwa pamoja halafu zinagawiwa bure kwa Watanzania. “Kila msanii ataimba topic yake kuhusu Antivirus, yaani atagonga jiwe lake kwa kutaja majina wahusika wa unyonyaji wa muziki wetu.

Watu ambao wanaua muziki. Tunagawa bure ili kutaka ujumbe ufike kwa Watanzania,” alisema Mkoloni halafu Sugu akaunga: “Ni bure na kazi yote itasajiliwa COSOTA kwamba haiuzwi. Mtu anaruhusiwa kutoa nakala na kumpa mwenzake. Itatoka Antivirus part I mpaka kumi kisha itakuja Antivirus Vol II. Wasanii wapo wengi na toleo la kwanza litakuwa na nyimbo 16.”
Ma-Lijendari wengine watakaokuwemo kwenye project ya Antivirus ni Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, G Solo na wengine.
**********************Miss TZ Yapewa tuition
Tuhuma dhidi ya Miss Tanzania ni nyingi, usisahau ile skendo ya ‘mapedeshee’, serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) iliamua kuandaa mkutano kazi wa kutathmini mwenendo wa Miss Tanzania kabla ya fainali za mwaka huu.

Wahusika wa mkutano huo walikuwa ni wadau wakuu ambao ni waandishi wa habari, wanaharakati, BASATA yenyewe, mawakala wa Miss Tanzania katika ngazi za kanda na ulichukua nafasi kwenye Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam Jumatano iliyopita.

Changamoto ya kuwatoa ‘mamisi’ usiku wakiwa kambini na kuwapeleka kwenye kumbi za starehe kisha kuwakutanisha na wanaume, kitendo ambacho kinaamsha vitendo vya ngono, iliibuliwa. Sakata la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu kuponda uamuzi wa majaji mwaka 2007 walipompa taji, Richa Adhia, pia malumbano ya Miss
Tanzania 1997, Saida Kessy dhidi ya Hoyce kwa matokeo ya Feza Kessy mwaka 2005 yaliibuliwa na kuonekana kuwepo kwa ukakasi wa uamuzi.

Hoja zote ziliwekwa kwenye kapu moja, Katibu Mkuu wa BASATA, Gonche Matelego akataka mabadiliko ili kuboresha mashindano, Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga akapokea hoja zote na kuahidi marekebisho.
********************
Makhirikhiri Ni stori ya kushtua
Mtawala mpya wa burudani ya asili barani Afrika, Moses Mapela a.k.a Shumba Ratshega na timu nzima ya Makhirikhiri, wameacha stori ya kushtua Kanda ya Ziwa kutokana na bonge la shoo ambalo walilidondosha pande hizo.

Shumba na timu ya Makhirikhiri ambao maskani yao ni Botswana, walipiga shoo kali kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Rocky City jana na Mei 29, walisababisha bonge la onesho ndani ya Shy Town. Anayeratibu mpango mzima wa tour ya Makhirikhiri Bongo ni Chande Mohamed ‘DJ Q’ ambaye

alituvutia waya jana na kutujuza maajabu ya Makhirikhiri ndani ya Lake Zone. “Wamefanya kweli, Mwanza mandhari ilibadilika, Shinyanga ni mshangao. Watu hawakuamini jinsi jamaa wanavyopiga ngoma na kucheza mitindo ya utamaduni kwa staili ya aina yake,” alisema DJ Q.

Sasa ni Dar, ladies & gentlemen mpo tayari? DJ Q anaweka tambarare kuwa Juni 4, 2010, hapa inamaanishwa Ijumaa ya wiki hii kwamba ngoma itakuwa inogile ndani ya Diamond Jubilee na Juni 6 a.k.a Jumapili, itakuwa shwari Uwanja wa Taifa. Timu ya Makhirikhiri, mbali na Shumba a.k.a Tajiri Mtoto, linaundwa na Philip Simon, Linda Mosimanagere, Olebile Edson, Nametso Sebele, na Motheo Johnson. *********************************
Askari Kanzu wa Oysterbay (kulia) akiwa ameshikilia bastola ya shabiki baada ya kunyan'ganywa
Shabiki akipanda gari lake huku akisema mbovu
Shabiki atoa bastola kwenye uzinduzi Extra Bongo
Shabiki mmoja ambaye hakunaswa jina lake mara moja, alimchomolea bastola mwenzake aliyekuwa katika geti la kuingilia katika Ukumbi wa Msasani Club, Dar baada ya kuzozana.

Ishu ilizuka wikiendi hii nje ya ukumbi huo, kulipokuwa na uzinduzi wa Bendi ya Extra Bongo chini ya Mzee wa Farasi Ally Choki. Chanzo cha njemba huyo kutoa bastola inadaiwa ni baada ya kuambiwa azime taa za gari lake, ndipo alipocharuka. Hata hivyo, mlinzi aliyekuwa mlangoni alionesha umwamba baada ya kumrukia na kumpora ile bastola kisha kupiga simu polisi ambapo baada ya muda mfupi, askari kutoka Kituo cha Polisi cha Oysterbay walifika na kumkamata na kuondoka naye kwenda kituo cha Polisi Oysterbay.
*************************************
compiled by mc george/Ijumaa wikienda

No comments: