Wednesday, May 26, 2010

PUMU HAIPATANI NA VYAKULA VYA MAFUTA

Kama tunavyosema kila siku, hakuna kitu kibaya kama mgonjwa kutokujua aina ya vyakula anavyopaswa kula na kuviepuka. kwa sababu bila kuwa na uelewa huo, uwezekano wa mgonjwa huyo kupata ahueni katika ugonjwa unaomsumbua, utakuwa mdogo sana.

Pumu ni miongoni mwa magonjwa yanayowasumbua watu wengi duniani, Tanzania ikiwemo. Ni ugonjwa ambao hauna tiba ya kuponya kabisa bali huwa na dawa ya kutuliza pale mgonjwa anapozidiwa.

Ili mgonjwa asisumbuliwe sana na ugonjwa huu unaoziba pumzi, tiba pekee ni kujua na kuepuka aina ya vyakula vinavyochochea, halikadhalika kujua aina ya vyakula vinavyotoa ahueni kwa mgonjwa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, vyakula vyenye mafuta mengi (high fat meal), huchangia matatizo katika njia ya hewa na hivyo kumfanya mgonjwa kupumua kwa tabu, tena hali hiyo huweza kutokea muda mfupi baada ya kula vyakula hivyo.

Kwa maana nyingine, mtu mwenye ugonjwa wa pumu anapokula vyakula vyenye mafuta mengi, kama vile nyama za kukaanga, chips, n.k, hufanya tatizo lake kuwa kubwa na gumu na kujikuta akibanwa na pumu mara kwa mara.

Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na watafiti nchini Australia, vyakula vyenye mafuta mengi husababisha hata dawa ya kutuliza pumu anayotumia mgonjwa (Ventolin ) ishindwe kufanya kazi yake sawasawa.

Aidha, utafiti huo umeonesha kuwa idadi ya wagonjwa wa pumu imeongezeka sana katika nchi za ulaya kutokana na kuongozeka kwa matumizi ya vyakula vyenye mafuta na kupungua ulaji wa vyakula vya asili.

LISHE YA MGONJWA WA PUMU (ASTHMA)
Baadhi ya vyakula vinavyoaminika kutoa ahueni na kuwa kama tiba kwa mgonjwa wa pumu ni pamoja na asali, juisi ya limau, mchanganyiko wa vitunguu swaumu na maziwa na mchangayiko wa abdalasini pamoja na asali. Vyakula hivyo vikiwa sehemu ya mlo wa mgonjwa kila siku, atapata ahueni ya ajabu.

Pamoja na kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, mgonjwa wa pumu anatakiwa pia kula kwa kiasi kidogo mlo wenye matunda, mboga za majani na vyakula vingine vitokanavyo na nafaka ambavyo hutoa ‘alikalaini’.

Aidha, wagonjwa wa pumu wanatakiwa kujiepusha na ulaji wa kiasi kikubwa cha wali, sukari, mtindi (yoghurt), unywaji mwingi wa chai, kahawa, pombe na vyakula vote vya kusindika au kwenye makopo.

Mgonjwa anashauriwa pia kufanya mazoezi ya kuvuta hewa safi na kuishi katika hali ya hewa isiyo na baridi, kunywa maji mengi mara kwa mara, kufunga kula (fasting) japo mara moja kwa wiki. Kwa kufuata masharti hayo, mgonjwa anaweza kuishi na pumu bila kusumbuliwa wala kutumia dawa kali kwa maisha yake yote.

11 comments:

Disminder orig baby said...

Ubarikiwe, hili ni tatizo kubwa sana katika jamii yetu ya leo.

Anonymous said...

thanx so much kwa info. yaani kijana wangu anasumbuliwa na tatizo hili na nitafuata masharti yako nione itakuwaje. God bless you luv

fadhili said...

PUMU au asthma si ugonjwa!!! ni upungufu tu wa maji mwilini(dehydration) kwa sababu watu wengi wanakunywa maji baada ya kusikia kiu. hatumwagilii bustani saa nane mchana, bali asubuhi kabla jua halijawa kali. www.maajabuyamaji2.artisteer.net/pumu

Unknown said...

Mimi nafanya kazi kwenye bekali. Ila nasumbuliwa sana na kifua nfanye nn
!?

Focus said...

Bado.kuna dawa huijui tazama dawa hii ndio kiboko na ni.mwisho wa tatizi

Malimao 4 ndimu 4 vitunguu maji 4 vikubwa viungo vya pilou pkt 4 na tangawizi kubwa 5 saga brenda zote ukiwa umetoa maganda na mbegu chuja anza kunywabjuice yako x 3 kwa siku athma itakuwa historia kwako dawa zw hospitali ninhatari sana

Anonymous said...

Vizuri sana
Ili tuishi mda mrefu twapaswa kupu
Nguza vyakula vya fati
Na kuongeza kula vyakula asilia

Anonymous said...

Kwer inasaidia ndug yangu

Anonymous said...

Jeeee pumu tunaweza kujiepisha vp

Anonymous said...

Niviungo vya pilau au vitunguu swaun hapo sijaolewa kiongoz

Anonymous said...

Je pumu inaendana na ulaji WA pili pili

Anonymous said...

Sasa SI uache kazi tu