Friday, June 4, 2010

IJUMAA SHOWBIZ



Wahuzunishwa na wizi wa kazi zao
Baada ya kuwarusha maelfu ya mashabiki wao waishio Kanda ya Ziwa mwishoni mwa wiki iliyopita Crew ya muziki wa asili kutoka Botswana ‘Makhirikhiri’ chini ya leader wao, Moses Malapela ‘Shumba Ratshega’ tayari iko Dar es Salaam kwa ajili ya kazi mbili kubwa, moja ikiwa ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee leo na nyingine kwenye Uwanja wa Uhuru, Jumapili.

Kabla ya shughuli hiyo kubwa, washkaji hao walidondoka ndani ya Ofisi za Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya Amani, Championi, Uwazi, Risasi, Ijumaa Wikienda na hili la Ijumaa na kunena kwamba watafanya kazi iliyowaleta kwa kiwango cha juu, ambayo haitasahaulika kwa wapenzi wa muziki huo hapa Bongo.

Kundi hilo ambalo lilitua Global katikati ya wiki hii likiwa na wasanii sita ambao ni Philip Simon, Linda Mosimaweghape, Olebile Edson, Sebele Nametso, Motheo Johnson na kiongozi wao Shumba Ratshega’, litasindikizwa na burudani kutoka kwa Wanne Star, Offside Trick na Omari Omari.

Kwa upande mwingine wasanii hao wamesikitishwa na wizi wa kazi zao uliofanywa na baadhi ya watu ambao wameivujisha albamu yake hapa Bongo bila yeye kuwa na taarifa.

“Hivi ni nani wanaofanya shughuli hii ya wizi wa kazi za wasanii, sisi tumeshangaa kukuta albamu zetu wakati hatukuwa na taarifa kama zipo nchini Tanzania,” alisema mmoja wa wasanii hao huku akiungwa mkono na wenzake.

Jamaa waliendelea ku-complain kwamba chakushangaza ni albamu yao mpya ambayo hata haijazama sokoni nchini Botswana but ipo Dar inauzwa kama njugu bila kutambua mazingira ya kuvuja kwake.

************************************************
Vita ya Chegge, Temba leo
Kutoka pande za TMK, vijana wawili waliotimiza jukumu moja zito wakiwa nje ya kundi lao, Amani James ‘Temba’ na Said Juma ‘Chegge’ leo Ijumaa ndani ya Club Sun Sirro pande za Sinza, Dar wana kazi ya kuwaambia mashabiki wao nini walichokuwa wanafanya kwa kipindi chote walichoamua kutangza vita hadi hii leo.

Nauzungumzia utambulisho wa albamu yao yenye jina la ‘Vita uwanjani’ ambayo watakuwa wanaitambulisha wakisimama steji moja na wakali kutoka Uganda na Kenya, yaani Michael Rose na Wahu waliyempa shavu ndani ya ngoma yao, ‘Mkono mmoja’.

Akipiga stori na ShowBiz juzi kati, Chegge alisema kwamba mbali na kuziweka hadharani ngoma zote zinazopatikana ndani ya albamu hiyo, wamejiandaa kufanya ‘sapraizi’ ambayo itawafanya ‘fans’ wao wakubali kwamba Vita uwanjani si kazi ya kitoto na kwamba wapo imara kuufanya muziki wa kizazi kipya uendelee kuwepo milele ili kufuta ule usemi kwamba game hiyo inaelekea kaburini.
Shoo hiyo imeandaliwa na Primetime promotions.
compiled by mc george/gpl

1 comment:

Unknown said...

Love them much! jamani give them support waache kuibiwa.