Monday, December 12, 2016

DALADALA LA ACHA NJIA NA KUJERUHI WATU WATATU TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

 Wananchi wakiangalia daladala lenye namba za usajili T 161 CRP lililoacha njia na kupinduka Mbagala Misheni kwa Bluda Dar es Salaam leo asubuhi na kujeruhi watu watatu.
Daladala likiwa mtaroni.

Na Dotto Mwaibale

WATU watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya daladala walikuwa wamepanda kutoka Temeke kwenda Mbagala Kuu kuacha njia na
kupinduka jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com Dar es Salaam leo asubuhi askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi wa Temeke ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa polisi alisema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 na nusu asubuhi.

Alisema daladala hilo liliacha njia na kutumbukia kwenye mtaro eneo la Mbagala Misheni kwa Bluda baada ya kuteleza kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha.

Alisema baada ya ajali hiyo wananchi walifika kutoa msaada kwa majeruhi ambao walikimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.

Alitaja daladala hilo kuwa ni lenye namba za usajili T 161 CRP ambapo alitoa mwito kwa madereva kuwa waangalifu wanapoendesha magari yao hasa katika kipindi ambacho mvua zinanyesha.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto ili kuzungumzia ajali hiyo zilishindikana baada ya kupigiwa simu ambayo ilikuwa ikiita pasipo kupokelewa.


No comments: