Monday, December 12, 2016

WAFANYABIASHARA SOKO LA MADENGE TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM WA JENGA KISIMA KWA NGUVU ZAO

 Fundi Martin Justine akitengeneza paa la kisima cha maji safi kinacho jengwa Soko la Madenge Temeke jijini Dar es Salaam kwa nguvu za wafanyabiashara. Ujenzi wa kisima hicho umegharimu sh.milioni 5.6.
 Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.
 Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.
 Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala'  akinawa maji yanayotoka katika kisima hicho ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia kubwa.


Na Dotto Mwaibale

WAFANYABIASHARA katika Soko la Madenge katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamejenga kisima cha maji salama chenye thamani ya sh.milioni 5.6 kwa kutumia nguvu zao na fedha za  ushuru wanaolipa.

Akizungumza na mtandao wa  www. habari za jamii.com Katibu Mkuu wa Soko hilo Shaban Malonji 'maarufu kama Wailala' alisema umoja walionao wafanyabiashara katika soko hilo ndio uliofikia maazimio ya kujenga kisima hicho chini ya viongozi wao.

" Binafsi napenda kuwapongeza wafanyabiashara wa soko letu kwa kuwa na umoja ambao umefanikisha kukamilisha ujenzi wa kisima hiki ambao utakamilika rasmi mapema wiki hii" alisema Malonji.

Malonji alisema kwa muda mrefu changamoto yao ilikuwa ni kukosa maji sokoni hapo ndipo walipokaa na wafanyabiashara wa soko hilo na kufikia maazimio ya kujenga kisima hicho ambacho kitakuwa kikitoa huduma ya maji sokoni hapo.

Alisema fedha za ujenzi wa kisima hicho zimetokana na ushuru wanaotoa wafanyabiashara hao na fedha zinazopatikana baada ya kulipa huduma ya choo cha kulipia pamoja na fedha za ushuru asilimia 10 wanazopewa na Manispaa.

No comments: