Tuesday, December 13, 2016

MKUTANO MKUU WA WANABLOGU TANZANIA 2016 UMEFUNGUA MILANGO YA MAFANIKIO

Disemba 05 na 06 mwaka huu 2016 ulifanyika Mkutano Mkuu wa Waendeshaji/ Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii nchini kupitia umoja wao wa Tanzania Bloggers Network TBN, uliofanyika
ukumbi wa PSPF Jijini Dar es salaam.

Siku ya kwanza ilikuwa mahususi kwa ajili ya semina kwa wanablogu hao juu ya namna ya kuendesha mitandao yao kwa ajili ya manufaa ya kijamii na yao pia. Siku ya pili ilikuwa mahususi kwa ajili ya mkutano Mkuu ambapo wajumbe wa mkutano huo waliwachagua viongozi wao ambapo Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (aliyesimama juu) na wasaidizi wake walisalia katika nafasi zao.
#BMGHabari


Mkutano huo ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, ambapo alitamka rasmi kwamba serikali inatambua mchango wa wanablogu nchini katika kuipasha jamii habari hivyo itaendelea kushirikiana nao akionya watendaji wa serikali hususani maafisa habari wa mikoni wasiotoa ushirikiano kwa wanablogu hao kuacha mara moja tabia hiyo.

Katika kilele cha mkutano huo, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye, ambaye alikiri umuhimu wa wanablogu nchini akisema kwamba, watatambuliwa rasmi kupitia kanuni za sheria mpya ya vyombo vya habari nchini ya mwaka 2016 na kwamba watapewa kadi za wanahabari (Press Card) ili kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi.

Kauli iliyowafurahisha wengi ni ile ya Waziri Nnauye aliyowakaribisha wadau mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa tuzo kwa wanablogu kwa mwaka ujao 2017 akisema wanafanya kazi kubwa hivyo ni vyema kutambua mchango wao kupitia tuzo.

BMG inawapongeza wote waliofanikisha mkutano huo, ikiwemo Bank ya NMB kwa ufadhiri wake, NHIF, PSPF, Kampuni ya bia Serengeti, Cocacola na TANAPA. Kwa pamoja tuienzi kaulimbiu ya mkutano huo, "Mitandao ya Kijamii ni Ajira, Itumike kwa Manufaa".
Kutoka kushoto ni Katibu wa TBN, Khadija Kalili, Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dk. Hassan Abbas na Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili na mjumbe wa kamati tendaji TBN, Klantz Mwantepele.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Katikati ni Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi na kushoto ni Katibu wa TBN, Khadija Kalili.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas na Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili.
Mwanablogu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wenzake.
Mwanahabari na Blogger  Frederick Katulanda 
Wanablogu wakiendelea kutoa mawazo yao katika kuijenga TBN
Wanablogu wanachama wa TBN
Wanablogu wanachama wa TBN
Tazama HAPA na HAPA ujionee.

No comments: