Tuesday, December 13, 2016

go yatangaza kuwasilisha dokezo la muhtasari kuhusu pendekezo la awali la kuuza hisa zake kwa umma



Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo balozi (mstaafu) Ami Mpungwe (katikati) akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji  wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez wakikabidhi kabrasha lenye mapendekezo ya kuomba kuorodhesha hisa katika soko la hisa la Dar Es Salaam (DSE) kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa soko hilo, Moremi Marwa.


Dar es Salaam – Desemba 8, 2016 –Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkononi ya MIC Tanzania Limited (Tigo) leo imetangaza rasmi kuwasilisha muhtasari  na maombi ya awali  katika Mamlaka ya Masoko ya Mitaji  na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kuhusiana na mapendekezo ya awali ya kuorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Uuzwaji wa hisa hizo unatarajiwa kuanza mara baada ya CMSA na DSE kumaliza mchakato wa mapitio kulingana na masharti yanayohusu soko la hisa.
Akizungumza wakati wa uwasilishaji huo Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Bwana Diego Gutierrez, alisema: “Tunayo furaha kutangazia umma kuhusu uwasilishaji wa muhtasari wetu  ili mchakato uanze rasmi na kwamba tutawapatia  wateja wetu, wafanyakazi wetu na Watanzania kwa ujumla  fursa ya kuwa wamiliki wa hisa ndani ya kampuni yetu.”
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya MIC Tanzania Limited, Balozi (Mstaafu) Ami Mpungwe aliongeza kuwa: “uwasilishaji huu ni hatua muhimu katika historia ya kampuni na kwamba utawapatia Watanzania wote fursa sawa ya kushiriki katika mtaji wa kampuni yetu katika siku za usoni. Tutafanya kazi pamoja na mamlaka za usimamizi kuhakikisha mchakato huu unafanyika ipasavyo.”

 Mwisho

No comments: