Thursday, December 7, 2017

MHANDISI KAMWELWE ATEMBELEA MRADI WA UPANUZI WA MFUMO WA UZALISHAJI NA UGAWAJI MAJI CHALINZE UNAOTEKELEZWA NA SERIKALI KUPITIA DAWASA



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI WA Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi Mradi wa maji awamu ya tatu ya upanuzi wa chanzo na mtandao wa maji wa Chalinze mkoani Pwani leo Desemba 6, 2017.


Mradi huo unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), upanuzi wa chanzo cha maji, ujenzi wa matenki na ulazaji wa mabomba, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji pamoja na ujenzi wa Ofisi mpya za Mradi.
“Mradi huu unahusisha  upanuzi wa mtambo wa kusafishia maji wa Chalinze ambao chanzo chake ni Mto Wami na lengo ni kuongeza uzalishaji kufikia mita za ujazo Elfu Tisa (9000) kwa saa kutoka mita za ujazo Mia Tano (500) kwa saa.” Amefafanua Mhandisi Kamwelwe.
Akifafanua zaidi Mhandisi Kamwelwe amesema, Mradi pia unahusisha ujenzi wa Matrenki 19, ulazaji wa mabomba ya ukubwa tofauti wenye urefu wa kilomita 1,022, ujenzi wa vizimba vya kuchotea maji 351 katika  vijiji na vitongoji vya Halmashauri za Chalinze na Bagamoyo Mkoani Pwani.
“Mradi huu ni Mkubwa na unahusisha pia baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Tanga na Morogoro katika wilaya za Handeni na Ngerengere.” Ameongeza Waziri huyo.
Aidha Mheshimiwa Waziri, alisema Wananchi wa maeneo yatakayofaidika na Mradi huo ambao ni Mkubwa ni pamoja na wakazi wa Manga hadi Tengwe katika Mkoa wa Tanga, mji na vitongoji vya Chalinze, na baadhio ya maeneo ya Bagamoyo na Kibaha Mkoani Pwani, wakazi wa maeneo ya Kizuka A na B, Tukamisasa, Lulenge, Visakazi hadi Bwawani  pamoja na Sangasanga A na B Mkoani Morogoro.
Maeneo mengine yatakayojengwa matenki ni pamoja na Pera, Pingo, Bwilingu, Msoga, Diozile, Lugoba, Mindutulieni, Saleni, Mazizi, Msata, Kihangaiko, Kilemera, Hondogo, Miono North 3, Kimange, Rupungwi na Manga.
Kati ya matenki hayo 19 mojawapo ni tenki kuu la Mazizi lenye uwezo wa kuhifadhi lita Milioni 2, kukamilika kwa ujenzi wa tenki hiulo kutafanya kuwa tenki kubwa zaidi kuliko yote Mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa Mhandisi Kmwelwe, Mradi utrakapokamilika utagharimu dola za KImarekani Milioni 41.36 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim yta nchini humo. Hata hivyo Waziri ameonyesha kukerwa kwake na kusuasua kwa mkandarasi kumalizia kazi hiyo kwa muda uliopangwa na kwamba kama asingefuata ushauri wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Wataalamu wa Wizara yake, basi leo Desemba 6, 2017 ilikuwa siku ya kuvunja mkataba wa Mkandarasi huyo. "Hata hivyo Mkandarasi baada ya kuahidi kukamilisha mradi Februari 8, 2017, tumeona tumuache hadi muda huo, lakini akishindwa hatuna njia nyingine ni kuvunja mkataba na kutafuta Mkandarasi mwingine." Alionya Waziri Kamwele wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye chanzo cha maji Mto Wami.
Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amemshukuru Waziri Kamwele na Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa nia yake ya dhati ya kuwaondolea kero ya maji wakazi wa Chalinze, na kwamba ana imani kubwa ya kukamilika kwa mradi huo baada ya kuulalamikia kwa muda mrefu bungeni kuwa umechelewa sana. "Mheshimiwa Waziri napenda nikushukuru sana na hasa Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Dkt. John Magufuli, kwa kazi nzuri ambayo Serikali inafanya katika kutatua kero za wananchi na hasa wapiga kura wa jimbo la Chalinze." Alisema Mhe. Kikwete. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe, (wane kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Majid Mwanga, Watatu kulia, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, (watatu kushoto),Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo, (wapili kulia), Mkandarasi wa Mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji kutoka kampuni ya WAPCOS Limited ya India, Mhandisi  P.G. Rajani na maafisa wengine, wamiwa mbele ya tenki la kusafishia maji linalojengwa chini ya mradi huo unaoendeshwa na Sewrikali kupitia DAWASA, kwenye chanzo cha Maji Mto Wami, Mkoa wa Pwani, Desemba 6, 2017


 Mhe. Mhandisi Kamwelwe, akizungumza jambo na Mhe. Ridhiwani Kikwete, walipotembelea chanzo cha Maji Mto Wami.
 Mbunge wa Bagamoyo, Mhandisi, Dkt.Shukuru Kawambwa, akimsikiliza Mhe. Waziri Kamwelwe, wakati wa ziara ya Waziri wilayani Bagamoyo kukagua ujenzi wa tenki la kuhifadhia Maji, Desemba 6, 2017. Tenkji hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 6.
 Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo, akitumia mchoro kuelezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa tenki la Maji Bagamoyo Mkoani Pwani, Desemba 6, 2017
 Mhe.Waziri Kamwelwe, akisalimiana na mmoja wa mafundi wanaojenga tenki la kuhifadhia maji Bagamoyo.

 Mkandarasi wa Mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji kutoka kampuni ya WAPCOS Limited ya India, Mhandisi  P.G. Rajani, akitumia mchoro kumueleza Waziri Kamwelwe, (wapili kuhsoto) na Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mwang'ingo, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi huo

 Taswira ya ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lita milioni 6, Bagamoyo Mkoani Pwani kama inavyoonekana Desemba 6, 2017

 Mhbe., Kamwelwe, (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.Majid Mwanga, (wapiili kulia) na Wakandarasi kutoka kampuni ya India ya WAPCOS.

No comments: