- Wateja 20 wapokea zawadi kemkem za pesa kwa kufanya miamala kupitia Tigo Pesa
Dar es Salaam, 8 Novemba, 2017- Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa leo imewatangaza na kuwazawadia washindi 20 wa promosheni yake ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’ inayoendelea katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka mpya ambapo wateja wanajishindia mamilioni ya pesa.
Washindi wanne (4) wamepata bahatiya kushinda zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 16 wakijaza mifuko yao na donge nono la shilingi laki tano (TZS 500,000) kila mmoja. each. Jumla ya shilingi milioni 12 zimetolewa kama zawadi kwa wiki hii.
Washindi wa zawadi za TZS 1 milioni ni wafanyabiashara Neema Fredrick Mosha, Fredrick Joseli Mponzi , Sefu Athumani Sefu na Hadija Mohamed Lukulumbale ambaye ni mama nitilie.
Washindi wa zawadi za TZS 500,000 ni Michael Joseph Moshi, Moses Muhonga Amuli, Saidi Khatib Kiko, Sylvester Michael Madaga, Aziza Ramadhani Ngozi, Evelyne Gwamaka Mwakyembe, Tumsifu Harold Temu na Sikudhani Constantine Mwenda. Wengine walioshinda TZS 500,000 ni Queentina Msafiri Mbwambo, Hilary Andrew Massawe, Ashura Ally Salim, Halima Saidi Shaabani, Fatuma Ally Makumbo, Halima Saidi Sangiwa, Jenifer Samuel Apolinale na James John Mkanula.
‘Tunatarajia kupata jumla ya washindi 153 katika kipindi cha mwezi mmoja wa promosheni hii. Bado tuna zawadi za thamani ya TZS 108 milioni kutoa kwa washindi 133,’ Meneja wa Wateja wa Tigo, Mary Rutta alisema wakati akikabidi zawadi kwa washindi Dar es Salaam leo.
Alibainisha kuwa pamoja na zawadi za kila siku, promosheni hiyo ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’ itakuwa na zawadi kubwa za mwezi TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni.
‘Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa ambao wanahitaji kutumia huduma ya Tigo Pesa kwenye simu zao ili kupata nafasi ya kushinda. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda,’ alisema.
Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya 70,000 waliosambaa nchini kote.
No comments:
Post a Comment