Nashukuru kwa kutuekea blog kuhusu afya zetu hongera kwa kuanzisha kitu tofauti,mimi nina swali kuhusu matibabu ya maji,kuna siku nilikuwa nasikiliza Radio One, kipindi fulani mama Teri alisema matibabu ya maji siyo mazuri!!!kwani kunywa maji mengi kwa kipindi kifupi binaadamu unapoteza Calcium nyingi mwilini kwa njia ya mkojo kuanzia hapo mimi nikaacha na nikawa siamini matibabu haya. Je haya ni kweli naomba jibu pls....!
Hilo ni swali kutoka kwa mmoja wa wasomaji wa Blog hii kuhusu makala yangu ya Water Therapy. (maajabu ya maji) Kwa kifupi dhana hiyo siyo sahihi. Kabla sijakujibu kitaalam zaidi, elewa kwanza maji yenyewe yana calcium hivyo katika hali ya kawaida huwezi kupungungukiwa calcium kwa kunywa calcium, labda tungefikiri kwa kunywa maji mengi utazidiwa na calcium.
lakini jambo lingine, Water Therapy ni zaidi ya kunywa maji tu, yenyewe kama ilivyo ni tiba inayoweza kuondoa matatizo ya upungufu wa calcium. unapokojoa unatoa sumu mwilini na maradhi mengine, na pengine calcium inayotoka ni kiwango kidogo sana ambacho hakipunguzi kitu mwilini.
Lakini kisayansi tunaambiwa kwamba Calcium inaratibiwa mwilini na Hormones aina mbili: parathyroid na calcitonin, ambazo hufanya kazi ya kuongeza na kupunguza calcium inayozidi mwilini. na ili hormones hizo zifanye kazi yake vizuri, mwili wako lazima usiwe na kasoro, na moja ya kazi za Water Therapy ni kuondoa kasoro na matatizo ya kiafya yaliyopo mwilini!!!
Asikudanye mtu, kunywa maji au water therapy haina madhara hata chembe, bali ina faida sana mwilini. hata siku moja mwili hauwezi kuishi bila maji.
Katika kuzungumzia suala hili kisayansi zaidi, hebu gonga link hii: (nakaribisha mjadala) http://www.merck.com/mmhe/sec12/ch155/ch155b.html
1 comment:
Nashukuru kwa majibu mazuri,nilikuwa sijapitia siku nyingi blog yako baada add.kunipote kule kwa michuzi nimeitafuta mpk nimeipata,ok nitajitahidi kunywa maj.Ombi mwambie Shigongo naye afungue blog tokea nimeondoka home nakosa magazeti yake tunayamiss hasa nilikuwa syakosi nilipokuwa huko mia mai zangu alizipata sihaba.
Post a Comment