Thursday, August 30, 2007

HII NI KASHESHE!


Na Richard Bukos
Mama mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Cecilia hivi karibuni alijikuta akipata kipondo cha nguvu baada ya kufumwa akila raha na mume wa jirani yake.

Tukio hilo la aibu lilitokea usiku wa manane wa Agosti 28 mwaka huu katika kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo Manzese karibu na Uwanja wa Fisi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, habari za dada huyo kufumaniwa na kupewa kisago zilitokana na kuvuja kwa siri ya ‘kumchuna’ na kufanya mapenzi na mume wa mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la mama Jane.

Ilidaiwa kuwa, mume wa mwanamke huyo ambaye jina lake halikupatikana alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kimwana mwingine na kwamba alikuwa akikutana naye usiku na kuponda raha kwenye kilabu hicho.

Siku hiyo ya tukio wagoni hao wakiwa katika mkao wa hasara, mke wa mwanaume huyo alitokea ghafla na kuanza kumtembezea kipigo, jambo lililoashiria kuwa alikuwa akimvizia mbaya wake.

Akionekana kujawa na hasira baada ya kuwabamba mama Jane alisikika akisema, “Si ulikuwa unakataa” alikatiza usemi wake na kumkunja mbaya wake huku akimwacha mumewe akitoweka kiaina.

Ghafla kilabu hicho kiligeuka uwanja wa ngumi na mieleka, huku mpambano ukimwelemea mgoni aliyeonekana kuyatungika ‘matap tap’ ya ofa ya mume wa mtu.

Hata hivyo baadhi ya wakata kilevi waliokuwa eneo hilo la tukio hawakuonesha kujali kwa kuamulia ugomvi huo, badala yake walisisitiza wagomvi waachwe wafundishane adabu.

Aidha baada ya sakata hilo kufikia tamati mama Jane alimwambia mwandishi wetu kuwa habari za kuibiwa mume alikuwa nazo siku nyingi na kwamba alikuwa akiwafuatilia ili awanase laivu.

“Nilikuwa na taarifa kuwa huyu ****** anatembea na mume wangu lakini nikawa sina uhakika, leo ndio nikaweka mtego wangu na bahati nzuri nimewabamba laivu,”alisema mwanamke huyo.

Aliongeza kuwa kwa tukio hilo ndiyo mwisho wa maisha yake ya ndoa kwani hawezi kuishi na mwanaume mhuni katika zama hizi za ugonjwa hatari wa UKIMWI.
(zaidi bonyeza hapa:http://www.globalpublisherstz.com/amani/)

No comments: