Wednesday, August 29, 2007

Niue nsiue?


Na Mwandishi Wetu
Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni alikumbwa na balaa la aina yake baada ya kupigwa vibaya kisha kuvuliwa nguo na kijana anayedaiwa kuwa ni mumewe.

Tukio hilo lilitokea saa 9.00 usiku, Jumamosi iliyopita katika eneo la Ukumbi wa disco wa Kahama Centre, uliopo Tarafa ya Makere mkoani Kigoma.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambacho kilikuwepo katika eneo la tukio, dada huyo aliiingia katika ukumbi huo kwa ajili ya kwenda kucheza disco bila kumfahamisha mumewe.
Habari zinasema kuwa akiwa ndani ya ukumbi huyo, alitongozwa na kijana mmoja ambapo alimkubalia na kupanga kutoka naye mara baada ya kumalizika kwa muziki.

Pamoja na makubaliano hayo, kijana huyo alimpatia mwanamke huyo shilingi 2,000 kama kichocheo pamoja na kumnunulia vinywaji ili asimwangushe.

Habari zaidi zinasema kuwa muziki ulipoisha, kijana huyo alimfuata dada huyo na kutaka waondoke, lakini alishangaa alipoambiwa kuwa hamjui.

Chanzo hicho kilisema kauli ya kutomtambua kijana huyo ilitokana na taarifa alizopewa msichana huyo kuwa mumewe alikuwa ametinga ukumbini hapo kumsaka.

“Sababu hasa ya kugoma kuondoka na kijana huyo ni baada ya kupata taarifa kuwa mumewe alikuwemo ndani ya ukumbi huo akimvizia baada ya kutonywa na wasamaria wema ,” kilisema chanzo hicho.

Habari zinasema kuwa muda mfupi baada ya mzozo, mume wa kijana huyo alifika sehemu walipokuwa wamesimama na kuwafuma wakibishana huku mwanamke huyo akidaiwa pombe aliyoinywa na shilingi 2,000 alizopokea.

Habari zaidi zinasema kuwa, mume huyo alimkamata kijana aliyekuwa na mkewe na kabla ya kumtandika makonde alichurupuka na kukimbia kusikojulikana.

“Kuona hivyo, mwanaume huyo alimgeukia mkewe na kumkwida huku akimpiga na kumlazimisha amtaje kijana aliyekuwa naye usiku huo,” kilisema hicho.

Kipigo hicho kiliendea kwa takriban dakika kumi ambapo alimshika msichana huyo na kumtoa nje kwa nguvu huku akimvua nguo zake na kubaki uchi.

Alipomfikisha nje aliendelea kumpa kisago huku akitoa maneno ya kashfa kwa kuwauliza watu waliokuwa wakishuhudia songombingo hilo; ‘niue ‘nsiue?’.

Habari zinasema kuwa kipigo kilipomzidi, dada huyo alidondoka chini na kugalagazwa kwenye mchanga, ambapo mmoja kati ya watu walioshuhudia aliweza kumpiga picha (kama inavyoonekana ukurasa wa mbele wa gazeti hili).

Chanzo cha habari kilisema kuwa msichana huyo aliokolewa na wasamaria wema baada ya kuona anaendelea kudhalilishwa.

Mwanamke huyo aliingizwa kwenye gari ya kukodi na kuondoka, haikufahamika alikopelekwa kwani mumewe alionekana akiranda sehemu hiyo kumsaka mbaya wake.

Habari zaidi zinasema kuwa tukio hilo limeacha gumzo kubwa mtaani hapo ambapo baadhi ya watu walikuwa wakimuonea huruma mwanamke huyo huku wengine wakisema alistahili kichapo kutokana na tabia aliyoionyesha.

Habari zaidi: http://www.globalpublisherstz.com/risasimchanganyiko/

1 comment:

Anonymous said...

Hivi huko Tanzania hakuna sheria za kulinda haki za binadamu kama wanawake?