Black Ryno
Safu yako ya mtaani Street Version, mwishoni mwa wiki iliyopita ilijadili na baadhi ya mastaa wa Bongo kuhusiana na filamu ya The Fake Pastors ambayo tayari imejipata umaarufu mkubwa kabla hata haijaingia sokoni.
Kama kawa safu hii huwa haipendi kuongea sana zaidi ya kuweka mada mezani, kisha wahusika wanaanza kuijadili. Watanzania hao wazalendo waliulizwa kwamba, wanaizungumziaje filamu hiyo bila kumsahau mtunzi Eric Shigongo, Je, ikiwa tayari inafahamika na mamilioni ya Wabongo, wanahisi itakuwaje, kimtazamo wao?. Hebu sasa tupate maneno yao.
Jina: Banana Zorro
Kazi: Mwanamuziki
Maoni: Mimi nafikiri filamu hii ya The Fake Pastors itakuwa bomba kwasababu wasanii wengi walioigiza ni wakali na wanauzoefu, kama Ray kila igizo au filamu anayoiigiza inakuwa safi, kwa hiyo mimi nachosubiri ni kuiona tu. Kwa upande wa mtunzi wa sinema hii nafikiri hakuna ubishi kwa sababu hadithi zake zote ni nzuri, naisubiri kwa hamu.
Jina: Nurdin Mohamed
(Check bud)
Kazi: Msanii wa maigizo
Maoni: Naweza kusema hii filamu ujio wake utakuwa wa kipekee kwasababu waliogiza ni moto wa kuotea mbali, nilivyoisoma katika vyombo vya habari imeigiziwa katika sehemu mbalimbali kwa hiyo itakuwa na ladha ya kipekee. Kuhusu huyo mtunzi kwasababu watu wanamjua habahatishi, naamini itakuwa na mandhari ya kipekee.
Jina: Mohamed Mwikongi (Frank)
Kazi: Msanii wa maigizo
Maoni: Hili picha litakuwa hatari kwasababu hii idea ni ya kipekee kwa hapa kwetu Tanzania. Mimi kama muigizaji najua itakuwa nzuri kwakuwa watu waliogiza mimi nawafahamu kiwango chao cha kazi kiko juu, kwa hiyo najua itatikisa Tanzania. Mtunzi nafikiri watu wote wanamjua jinsi alivyokuwa mbunifu na yuko makini katika kazi.
Jina: Nicholaus Haule
(Black Rhyno)
Kazi: Mwanamuziki
Maoni: Binafsi siwezi kusema itakuwaje kwasababu bado sijaiona, nitakapoiona nitatoa maoni yangu mengi tu. Kuhusu mtunzi wa hiyo muvi cheche zake nazijua kwa hiyo sina ubishi naye kwani yuko juu katika hadithi.
No comments:
Post a Comment