Monday, October 8, 2007

Amanda: Nilimsaliti Dk. Cheni


uigizaji anayekuja juu nchini, Tamrina Mohammed ‘Amanda’ (PICHANI), juma lililopita aliifungia ‘breki’, Abby Cool & MC George Over The Weekend na kufanya bonge la ‘confession’.

Si unajua Amanda ndiye aliyekuwa ‘akichati’ kimahaba na galacha wa maigizo Bongo, Muhsin Awadh ‘Dk. Cheni?, basi ameibuka na kusema kwamba ingawa walikuwa wakitoka na kuahidiana kufunga ndoa, lakini alikuwa anamfunga kamba mshkaji.

Amanda alitonya kwamba wakati ‘akiduu’ na Cheni, wakati huo huo, alikuwa na jamaa yake mwingine aliyekuwepo ‘mamtoni’ ambaye ndiye wake wa kufa na kuzikana, kwahiyo alikuwa akimcheza shere kimtindo daktari wetu.

“Huo ndiyo ukweli wangu, kwahiyo mimi sikuwa nampenda jamaa ‘kiviile’, tena nimefurahi ameoa, ili na mimi nitulie na mtu wangu ambaye nampenda kwa dhati na sasa hivi tunaandaa mikakati ya ndoa.

“Yaani ni furaha tu kwangu, na kwa kuongezea ni kwamba ‘kidume’ wangu ameshatua Bongo kutoka UK,” alilonga Amanda.

Hivi karibuni msanii mwenzie Muhsein Awadh, maarufu kama Cheni aliona demu mwingine, hali iliyogusa Amanda na ilidaiwa alipata 'kapresha' flani hadi kulazwa.

No comments: