Monday, October 8, 2007

JOTI ASAKWA NA JWTZ, NOMA!

Msanii wa kundi la vichekesho, maarufu Ze Comedy, Lucas Mhuvile ’Joti’ anadaiwa kusakwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kile kinachoelezwa kuvaa sare za jeshi hilo.

Taarifa za kiuchunguzi kutoka ndani ya jeshi hilo, zimedai kuwa baadhi ya maofisa wa ngazi ya juu wamechukizwa na kitendo cha msanii huyo kuvaa sare hizo licha ya kupiga marufuku.

Msanii huyo ambaye kikundi chake kimekuwa kikirusha vichekesho vyake kupitia Kituo cha Televisheni cha East Africa, amekuwa akivaa nguo hizo mara kwa mara.


Septemba 29, mwaka huu, Joti alivaa nguo hizo mbele ya viongozi wa serikali wakiwemo maofisa wa jeshi hilo na wa usalama katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Mfuko wa Uwajibikaji Uadilifu na Uwazi ambako walialikwa kuburudisha.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya viongozi waliokuwepo walianza kuhoji uhalali wa msanii huyo kuvaa nguo hizo wakati wasanii wengine kama vile Gwamaka Kaihula ‘GK’ alishakamatwa na kushikishwa adabu kwa kosa hilo.


“Inashangaza kuona sare za jeshi zinafanyiwa mzaha na vikundi vya vichekesho, hii ni dharau kwa majeshi yetu, tutamsaka ili kumchukulia hatua kama ataendelea kuvaa,” alisema afisa mmoja wa jeshi hilo aliyekuwepo katika viwanja hivyo alipoongea na mwandishi wetu.

Kufuatia hali hiyo, Joti aliulizwa kapata wapi ubavu wa kuvaa sare za jeshi hilo wakati ilishapigwa marufuku?

Msanii huyo hakutoa majibu badala yake naye aliuuliza swali;

Mwandishi: Joti, habari?

Joti: Nzuri.

Mwandishi: kuna madai kuwa wewe unadharau jeshi la wananchi, ndiyo maana unavaa sare zao bila kuogopa. Nini ukweli wa hilo?

Joti: Kwanini unaniuliza hivyo?

Mwandishi: Kwa sababu mwanamuziki Gk alishakamatwa pia Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ alishapigwa mkwara kwa kuvaa sare zao.

Joti: (badala ya kujibu alikata simu, alipopigiwa tena hakupatikana).

1 comment:

Anonymous said...

TUNAOMBA PICHA ZA JK JANA
UWANJA WA NDEGE