Monday, October 8, 2007

STREET VERSION:Tibaigana alia na vyeti ‘feki’ vya Ukimwi


TACAIDS waingia mitini, Kandoro bize na vikao

Mwishoni mwa wiki iliyopita ‘Street Version’ iliamua kujitoa muhanga kwa kuwaibukia baadhi ya viongozi wa serikali na Taasisi ya TACAIDS ili kupata maoni yao baada ya Gazeti la The Bongo Sun hivi karibuni kuchapisha habari ya kusikitisha, iliyosema kwamba kuna baadhi ya madaktari wa Angaza wanaihujumu taasisi hiyo kwa kutoa vyeti feki vya Ukimwi.

Lengo ni kutaka kusikia kauli za viongozi, pia kuleta usawa katika safu hii baada ya kuongea na Watanzania wa kawaida pamoja na mastaa mbalimbali katika mada zilizopita. Kamishna wa Kanda Maalum Mkoa wa Dar es salaam, Alfred Tibaigana ndiye alikuwa wa kwanza kutiliwa timu na safu hii, akiiongelea ishu hiyo, yafuatayo chini ndiyo maoni yake.

“Kwanza kupima ukimwi ni hiyari, halazimishwi mtu na hao madaktari wanaofanya hivyo wananisikitisha sana, vilevile namlaumu sana huyu mtu anayefanya hivyo kwa ajili ya kuwadanganya watu.

“Yaani mtu na akili zake timamu anatoka kwake hadi katika kituo cha kupima Virusi vya Ukimwi halafu anachukua pesa anampa daktari ili ampe cheti kilichoandikwa yuko safi (Negative), nahisi akili zake si nzuri kwa sababu anataka aendelee kuwaua wasio na hatia”.

“Naweza kusema wote ni wahalifu lakini yule anayemlazimisha daktari ni muhalifu zaidi kwa sababu anambembeleza ili akubali ili yeye afanikishe azma yake wakati anajua kabisa kipindi hiki Rais anasisitiza kila siku watu wakapime wajue afya zao, sasa iweje mtu ana nunua cheti feki?’, Alihoji Tibaigana aliyekuwa ameibukiwa ofisini kwake.

Baada ya kutoka kwa Tiba, Street Version ilikata mitaa na kuibukia kunako Taasisi ya kupambana na Ukimwi, TACAIDS ili ipate kuongea na Mwenyekiti wake, Fatma Mrisho, lakini bila kutegemea ilifahamishwa kwamba kiongozi huyo yuko nje ya nchi kikazi na ajabu zaidi wasaidizi wake walichomoa kuongelea ishu hiyo. Hapo ndipo safu hii ilipojiuliza kwamba, ina maana mwenye ‘masofa’ huyo hana kaimu?

Baada ya kuachana na TACAIDS, safu hii ikaibukia Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, zilizopo Wilayani Ilala ili ipige stori na Abbas Kandoro, lakini jibu lilikuja kwamba mheshimiwa huyo yupo kwenye kikao. Baada ya kugonga mwamba kuongea na viongozi hao wawili, safu hii inakuahidi wewe msomaji kwamba, bado itaendelea kuwatafuta tena, pindi watakapopatikana maoni yao yatachapishwa hapa.

No comments: