Sunday, October 7, 2007

Yakuza Mobb kuchomokea kwenye TV


wasanii wawili wakali wanaofanya kundi liitwalo Yakuza Mobb, Mbwana Khamis a.k.a MB wa Yakuza na Geoffrey Jilla a.k.a Jilla Jeff wameiambia Abby Cool & MC George Over The Weekend kwamba, kazi mpya yenye jina la ‘I Know U Know’ ambayo waliiachia redioni na kushindwa kufanya vizuri sasa wataitoa kupitia video.

Wakiongea kwa kupokezana vijana hao ambao wamemshirikisha Mohamed Mbwana ‘MB Dog’, walibainisha kwamba, kazi hiyo ya kukamilisha video ndiyo iliyowafanya wawe kimya kwa muda tangu walipoachia pini hilo redioni, huku wakisikika kwenye remix ya wimbo Si ulinambia wa MB Dog.

Kitu cha msingi vijana hao walisema kwamba ili kuisimamisha zaidi kazi hiyo wanatarajia kuitambulisha kwa mashabiki kunako shoo itakayofanyika siku ya Idd Mosi ndani ya ukumbi wa GFC Motel uliyopo Chanika, Dar es Salaam, sambamba na mchizi wao, MB Dog. “Katika upande wa mashine tutakuwa na mchizi wetu DJ Sos P” alisema Jilla Jeff.

No comments: