Sunday, October 7, 2007

WASHIRIKI C2C PRESHA JUU!

Fainali C2C imekaribiaktoba 10 mwaka huu, yaani Jumatano ya wiki hii ndiyo siku ya kuwapata washindi wanne ambao watakula shavu la kutangaza katika kituo cha televisheni cha C2C cha Dar es Salaam, kupitia shughuli ambayo itafanyika mbele ya Waziri wa Kazi na Maendeleo ya vijana, Mhe. John Chiligati ambaye atakuwa mgeni rasmi, Christopher Lissa anaandika.

Ndani ya safu hii Meneja wa Kampuni ya QSSP Group Ltd ambao ndiyo waandaaji wa shindano hilo, Bahati Sigh alitamka kwamba maandalizi ya fainali hiyo yanaendelea ‘fresh’, huku washiriki 12 waliosalia wakiendelea kujifua kikamilifu.

“Katika hizi siku chache zilizobaki hakutakuwa na mchujo kwa washiriki waliosalia, bali watachuana siku hiyo ya fainali. Siku hiyo ya fainali washiriki nane watatajwa kutoka, wanne watakaobaki ndiyo watakuwa washindi wetu.

Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd ambao ni wachapishaji wa magazeti pendwa ya Ijumaa, Risasi,Uwazi,Championi,Ijumaa Wikienda, Amani, S&C Magazine na The Bongo Sun.Wadhamini wengine ni Zizzou Fasion, Hoteli ya Regency Park na kampuni ya ulinzi ya Aurora.

No comments: