Friday, October 26, 2007

SHOWBIZ


Akudo kupekecha na Banza, Choki

Shabiki gani wa muziki wa dansi ambaye bado hajalisikia jina la Akudo Impact? Kama wapo ni wawili au watatu, nasema hivyo kwa sababu hata wale wanaouzimia muziki wa kizazi kipya nimewahi kuwashuhudia wakijichanganya katika shoo za bendi hiyo.

Ishu zilizoifikia ShowBiz zinasema kwamba, washikaji hao ambao staili yao yenye jina la Pekecha Pekecha inabamba ile mbaya, Oktoba 31 mwaka huu watajitambulisha wilayani Temeke ndani ya Ukumbi wa Luxury Pub, baada ya hapo wataelekeza nguvu zao kwa wasanii Banza Stone na Ally Choki.

Namaanisha kwamba washikaji watapiga shoo ya kutosha kunako utambulisho wa albamu yenye jina la ÔSisi ndiyo sisiÕ ya kwao Banza na Choki utakaofanyika ukumbini, Diamond Jubilee Novemba 3, mwaka huu kwa mashambulizi ya burudani nyingine za nguvu kutoka ndani ya kikundi cha taarabu cha Jahazi Asilia.

Mbali na Jahazi, TMK Wanaume Halisi wakiwa na tuzo ya kiongozi wao, Juma Nature watapamba jukwaa na staili yao, Kung-fu Flex, yote ikiwa ni kuwasapoti kaka zao hao waliyopo kwenye game ya dansi kitambo. Mzee Muhidin Maalim Gurumo kutoka ndani ya Bendi ya Msondo pia atakuwa kivutio kwa mashabiki pale atakaposimama jukwaani na vijana hao.

Albamu hiyo, Sisi ndiyo sisi tayari imetambulishwa na nyimbo kadhaa ukiwemo Salary yangu, pia imewashirikisha wasanii wengine kibao wakiwemo Msafiri Diouf na Kitokololo wa FM Academia.

No comments: