Monday, January 28, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Du! Mr. Nice aibukia Tegeta!

Akiwa na bendi yake, Group Jambo ambayo inaunguruma kwa miondoko ya muziki wa dansi, msanii Lucasi Mkenda Mr. Nice baada ya kupotea kwa muda katika game hiyo ameibukia maeneo ya Tegeta, Dar es Salaam ambako atakuwa akifanya maonyesho yake, Issa Mnally alimbamba.

Akipiga stori na safu hii muda mchache baada ya kushuka jukwaani msanii huyo alisema kuwa ameamua kuibukia huko ili kuvunja ukimya wa kwamba kaishiwa kisanii, atakuwa akifanya shoo Tegeta kila siku ya Jumatano.

"Sasa nimeamua kuwafuata mashabiki wangu wa huku Tegeta kuanzia leo, nitakuwa nikifanya vitu vyangu kwa nikishirikiana na hawa wenzangu kila siku ya Jumatano," alitamka msanii huyo, muasisi wa staili ya Takeu nchini.

Katika onyesho hilo la kwanza Mr. Nice alionesha kwamba bado hajaishiwa kisanii kwa kufanikiwa kuwarusha kwa sana mashabiki wengi waliojitokeza kumshuhudia yeye pamoja na bendi yake mpya.

Thea:Mapenzi na mastaa ni kama usingizi

Msanii wa sanaa za maigizo na sinema, Ndumbagu Mesayo a.k.a Thea ndiyo alipiga stori na Hot Corner, mwishoni mwa wiki iliyopita. Kama kawa alikutana na maswali ya kila aina, bila kusahau yale ya kizushi yaliyoshushwa na Catherine Kassally.

Hot Corner: Ungependa uwe mama wa watoto wangapi?

Ningependa kuwa mama wa watoto watatu, wa kwanza wa kiume na wawili wawe wa kike ingawa sichagui jinsia.

Hot Corner: Muigizaji gani wa Tanzania unayemzimia kwa kazi zake?

Wapo wengi, lakini ninayemzimia sana ni Riyama.

Hot Corner: Wewe kama msanii, kioo cha jamii unaelewa vizuri maambukizi ya gonjwa hili hatari la Ukimwi. Je, umewahi kutumia kondomu na mpenzi wako?

Natumia kondomu na mpenzi wangu, ila tukishapima tutaacha kutumia.

Hot Corner: Ushawahi kufanya mapenzi na supa staa yeyote?

Sijawahi kufanya mapenzi na staa yeyote kwakuwa nafahamu mapenzi na mastaa ni kama usingizi, kufumba na kufumbua hakuna mapenzi. Kwakuwa nimeishi muda mrefu katika sanaa nimeona mambo mengi, ndiyo maana sitathubutu kufanya hivyo.

Hot Corner: Unafikiria nini kuhusu maendeleo yako kimaisha?

Mimi kama msanii, ndoto zangu ni kujiendeleza zaidi kisanii. Hivi sasa tayari nimeshatengeneza filamu yangu iitwayo Ukungu, pia nafikiria kuwa na studio yangu ambayo itasaidia kuendeleza soko la filamu nchini.

1 comment:

Anonymous said...

Halafu mnalalamika hamuolewi,kutuza bikira hamtaki.